Home || The Aggressive Vision || Prophetic Word Of The Lord || On Line Library || Current Articles and What's New
Free Literature || Visions from The Lord || More About ACMTC || Contact 

Maneno ya Unabii.

(Prophetic Messages)

 

 

Kuhusiana na Dini

(Concerning Religion)

 

 

Aggressive Christianity Missions Training Corps

 

MWILI HAUTAINGIA

(Flesh will not enter. Issue 10 WOS 12-16-89 pg. 21)

 

Zaidi nawaambieni kwamba nimewaleta kwenye sehemu, ndiyo nimewaleta kwenye sehemu ambapo niliwaambia mwili hautaingia ndani yake. Na nawaambia msichukulie kiwepesi jambo hilo, kwani nawaambia nitafunua wazi miliki nyingi za mwili wa kidini unaojiweka kama wa kiroho, nasema kwamba wakati nitakapovifunua vitu kama hivyo ,uwe makini navyo na usivifunike na kuvifanya kama kwamba ni vya kiroho.

                                       

Kwa maana nasema kwamba nimewaambia hakuna vitu vya kimwili vitakavyoingia katika uelekeo wa kiroho pamoja

nami. Nawaambia usiku huu ya kwamba toba inamaanisha kwamba unafanya mabadiliko katika Mimi. Na unapokuja kwangu na kutubu na wakati unapokiri dhambi zako inamaanisha umebadilika.

 

Nawaambieni msitubu kwangu halafu mkaendelea na kufanya tendo lile tena au jambo lile tena. Kwani nawaambia jambo hilo halinifurahishi kwani ni kunifanyia utani na unafanya utani wa toba wakati unapofanya jambo hilo lisilo la akili.

 

Kwani nawaambia toba ni jambo muhimu na nisinge tamani mtu alichukulie kiwepesi. Lakini nasema wakati mmetenda dhambi na wakati mmefanya makosa na mkaona hivyo nasema badilikeni kwani kwa mabadiliko hayo ndiko kwenye toba ya kweli ya moyo.

 

MUNGU SIO DINI

(God is not a religion)

 

Nawaambieni wakati mwanadamu anandaa utaratibu wake mwenyewe wa kimwili ili uonekane na wanadamu wengine, hilo ndilo atakalo bakia nalo. Kwa maana nawaambia mwanadamu huyo hawezi kuishi na kufangamana na mwongozo wa Roho.

 

Nasema watakuwa na kanuni zao tu za kidini za kuwafanya wengine wawaone, ili wawafanye wengine wawatamani, wengine watakashifu kanuni hizo. Lakini nawaambia hawatanipata Mimi kwani nawaambieni Mimi Bwana Mungu wenu siwezi kufungiwa ndani ya viboksi vya taratibu za dini zenu.

 

Kwani nasema Mimi ni Mungu aishie. Nawaambia Mimi si wa kidini. Dini ni mipango ya kibinadamu ya ubunifu, kufikiria isiyo kweli. Nasema Mimi sio dini . Mimi ni Mungu aliye hai.

Nasema naishi kila siku nasema nawalisha watu kila siku, nasema siku zote nabubujika kwa watu wangu. Nawaambieni siwezi kufungiwa katika boksi na kufungashwa na kuwekwa pamoja katika kanuni za dini.

 

Kwani nawaambieni watu wangu Mimi sio dini. Mimi daima natembea, daima natoa uzima wangu, daima natoa ufunuo mpya kwao ili waweze kusonga mbele kwangu, nasema wakati mwanadamu anapojistawisha katika dini, kimsingi anajistawishia kifo. Kwani nasema Mimi Mungu niliye hai sifungamani na dini. Lakini nasema daima niko hai kwa watu wangu ndio kwa watu wangu wanaonifuata katika kweli.

 

Nawaambieni watu wangu msiruhusu dini iwe mfumo wenu wa kuishi na ijistawishe ndani yenu.Kwani sitamani nyie muwe watu wa mfumo wa dini. Lakini nasema natamani kuwaona mnaongozwa katika uzima wangu. Kwani nyie ni wangu nasema Mimi ni hai. Nasema natamani watu walio hai.

 

Nasema ishi na ufungamane nami, nami nitawafanya kusonga mbele. Nasema usimruhusu mtu yeyote akufunike chini ili uwe wa kidini. Lakini nasema endelea kunifuata Mimi.

 

WAVAAO DINI KAMA KINYAGO

(Religious masks. Issue 32 WOS 1992 pg 6)

 

Nawaambieni wakati Mimi Bwana Mungu wenu ninapomwita mtu mume au mke, nawaambieni nitakitengeneza chombo kama nionavyo vyema Mimi. Nasema nitakitengeneza chombo kama nionavyo vyema Mimi na nitaweka kitu ndani yake nitamiminia uzima, nasema ntakimiminia nguvu na utukufu kama nionavyo vyema Mimi.

 

Nasema mtu yeyote ambaye amejitengeneza mwenyewe nasema mtu aliyejitengeneza kwa tamaa zake, kwa kazi zake mwenyewe, nasema huyo si mtu wangu. Kwani nawaambieni mtu ninaye mtengeneza atakuwa amechongwa kwa mkono wangu. Nasema wakati watu watakapo jaribu kuchonga nafsi zao katika sura na mfano wangu nasema watajiletea kifo.

 

Nasema wanajiletea kitu kile ambacho hakiishi kwani nasema hakuna binadamu anayeweza kuigiza nguvu yangu, hakuna mtu anayeweza kuigiza utukufu wangu na nasema wakati watakapo jiweka nafsi zao namna hii au ile au nyingineyo nasema wanakuwa wanavaa vinyago vya dini.

 

Nasema ni wanafiki wa kidini nasema wao ni Mafarisayo na Waandishi. Kwani nawaambieni kwamba hao hawakujishuhulisha mbele zangu na kuvunjika katika mikono yangu na kuchongwa kwa mkono wangu. Nasema hao hawakubaliki kwangu, nasema wamekufa. Lakini nawaambieni kwamba kile ambacho mimi Bwana Mungu wenu nakichonga, nasema chombo kama hicho kiko hai.

 

 Nasema hai katika nguvu yangu na utukufu. Nawaambieni watu wangu msiangalie wavaa dini kama vinyago na kuwafikiria wako hai. Kwani nawaambieni wamekufa. Nawaambia wame kufa katika maovu yao nadhambi zao.

 

Nasema wamekufa katika unafiki wao, nasema hawako hai, kwani nasema wamejichonga nafsi zao katika uovu. Nasema furahini wakati nitakapo wachonga nasema furahini wakati nitakapo wavunja vunja ninyi na wakati nitakapo waunda. Kwani nasema kwa jinsi hiyo utaishi nasema hivyo mnaishi, hivyo mwaishi kwani Mmi ni Mungu aliye hai, nanyi mwaishi ndani yangu.

 

SHUKRANI KWA MUNGU

(Give thanks to God)

 

Nasema nishukuruni kwamba Neno langu liko hai na Neno langu sio mfu. Nasema daima Neno langu linaishi na Neno langu ndicho kiini cha uzima. Nasema nishukuruni watu wangu.

 

MADHEHEBU KATIKA UFUNUO MDOGO

(Denominations in every small revelation Issue 15 WOS pg 8 1-14-90)

 

Nasema wanadamu husimama na wanajenga dhehebu kwa kila ufunguo mdogo ninaowapa. Nasema msijenge dhehebu katika kila ufunuo wangu mdogo. Lakini endeleeni kunipokea Mimi, endeleeni kuniruhusu Mimi niishi ndani yenu katika ukamilifu wangu wote.

 

 Endeleeni kuniruhusu Mimi niwalete katika hali isiyo na mwisho. Kwani nawaambieni Mimi Bwana Mungu wenu sitamani watu wa jinsi hiyo, kwa muundo mdogo namna hiyo

 

DINI YAKO IWEKE CHINI YA MIGUU YAKO.

(Put your Religion under your feet. Issue 36 WOS 1992 pg 20)

 

Nawaambieni je, kwenu inajalisha, ni utawala upi ninaotamani kuwapeni? Nawaambieni nyie nitiini tu, nasema kama natamani kuwapa utawala fulani, nasema nyie nitiini tu kirahisi na mchukulie hivyo kwani nawaambieni sio kazi yenu ya kuwafanya wanafunzi wa kidini. Nasema si juu yaenu kuwa wahukumu wa kidini. Lakini nawaambieni ni juu yenu kutii , nasema chukua dini yako na iweke chini ya mguu yako. Nasema hainifurahishi.

 

MUNGU HUWACHUKUA WATU WAKE KATIKA NJIA ZA MWINUKO

(God takes His people in highlands. Issue 36 WOS 1992 pg 20)

 

Nasema usione aibu au kuzidi sana kuwa mtu wa kidini, nasema msione aibu au kuzidi sana kuwa mdini, kwani adui atajaribu kuwastawisha nasema atajaribu kuwateka katika mtego mwingine mahali pasipofaa, nasema atajaribu kuwanasa. Nasema atajaribu kuleta kwenu mabandeji ya kidini, kwamba kwa kufanya hivi, bila kufanya hivi na hivi.

 

Wewe hufanyi kazi ya Injili au kutimiza utume. Lakini nawaambieni kwamba huyo ni mwongo, kwani nawaambieni Mimi huwachukua watu wangu katika njia za mwinuko na katika mahali pasipo na njia kwa jinsi yoyote inayonifurahisha Mimi.

 

Nasema nawapeleka watu vijijini na katika vitongoji kwa jinsi yeyote inayonipendeza m

Mimi. Nasema nawasukuma watu wangu waende nje ili neno langu liweze kwenda nje.

 

Nawaambieni msimruhusu awafanye watu wa kidini, nasema msimruhusu awaweke katika viboksi vidogo. Nasema msimruhusu awafungie ndani, lakini nawaambieni endeleeni mbele katika kunitii na nasema mtatimiza kila kitu ambacho Mimi nakitamani kwani nawaambieni njia zangu ni kuu kuliko njia za mwanadamu.

 

Nasema njia zangu sio kama za wanadamu, nasema wanadamu hufikiri wanalo neno langu likiwa limefungashwa, nasema hawana lolote ila mavumbi makavu, kwani nawaambia hawanalo Neno lililo hai.

 

Nawaambieni wale watu wanitiio Mimi, nasema na kunifuata, nasema watakuwa na neno lililo hai. Nawaambia jitumeni katika eneo lolote nitakalo kuonyesha na nasema matunda yatatokea katika eneo hilo. Nasema matunda yatatokea katika eneo hilo.

 

Ninawaambia watu wangu msiwe watu wa kidini kupindukia bali nifuateni Mimi. Nasema nitawaongozeni katika njia za mwinuko na mahali pasipo na njia. Nasema nitawaongoza katika vijiji na vitongoji, nasema nitawaongoza mbele mlitangaze Neno langu.

 

Nasema msidhani mnatakiwa kuvaa mavazi mapana ya kidini (kama makanzu) kwani nawaambieni Mimi Bwana Mungu wenu nitawaongoza katika tabia na taratibu nitakayo pendelea ili kuwafikishia watu wangu neno langu.

 

Nasema furahini katika Mimi kwani Mimi huleta mambo mapya kwani siko kama wanadamu, nasema siko tu kimya na kutulia na kukaa na kukwama; lakini natembea, nasema nishukuruni kwamba mnamtumikia Mungu aliye hai.

 

JINSI NENO LA MUNGU LILIVYOENEA

(How the Word of God was spread)

 

Nawaambieni kabla binadamu hajaamua kuyafungia maneno yangu yote katika boksi na kuanzisha dini. Nasema mnafikiri Neno laangu lilisonga mbele kwa vipi? Nasema lilisonga mbele katika sehemu za masokoni, nasema lilisonga mbele katika sehemu za kawaida zilizoandaliwa, nasema lilisonga mbele katika sehemu zenye mikusanyiko ya watu, nasema mahali ambapo watu walikuwa mbele.

 

Nasema msimruhusu adui kuwajengea picha nanyi mkadhani iliwezekana kufanyika tu katika sehemu tu zilizofungiwa maalum, lakini nasema kaeni hali mmefunguka kwa Roho wangu, kwani nawaambieni Roho wangu anaweza kwenda katika mazingira ya aina nyingi kwani nawaambieni Niko hai. Nasema Niko hai, nasema zifikirini nafsi zenu wenyewe, nasema mara ya kwanza mlipolisikia Neno langula uzima nasema je, bado mlikuwa mmeng’ang’ania kwenye vifungo vya kanisa?

 

 Nasema mlikuwa kwenye mipangilio iliyo sahihi? Nasema au Neno langu nilikuja kwenu pale mlipokuwa? Nasema je, Neno langu liliwajia katika mazingira yasiyoeleweka, nasema je, lilikuja kwenu katika mazingira yasiyokubalika kwa wanadamu wale waliozama katika dini? Nasema ndivyo lilivyofanya.

Nasema Neno langu li hai , nasema ntalituma nje kupita vyombo vilivyo hai. Nasema nalituma pale panaponipendeza Mimi. Nasema nishukuruni kwa msukumo mpya ninaowasukuma kwao. Nasema nishukuruni kwa hilo kwani nasema nitawabarikini.

 

Lakini nasema hamwezi kuzipata bila kuzi hangaikia nasema msipofushwe na kuwa wajinga, nasema hamwezi kuzipata bila mahangaiko lakini nawaambieni nitawapa nchi.

Nawaambieni kama mngeenda katika mazoezi, nasema utume ambao ungeugundua ni wengi kuwa wakavu, kukondeana katika mvinyo. Nasema hawaleti matunda, hawaleti uzima, nasema wao wamefanywa uchungu, nasema wamejistawisha hali zao zisizo sawa.

 

Je, wameolewa na Mimi? Hapana nasema wameolewa na kazi zao, lakini nasema kazi zao zitajakuwa si kitu, kwa maana nasema kazi zao hazija jaa uzima wangu wala utukufu wangu. Nasema wako kidini tu vitu vya kutazamwa na wanadamu. Nashukuruni kwamba Mimi ni Mungu niliye hai.

 

 

MTU HUWEZA KUONEKANA MWANADINI MZURI ILA KWA MUNGU AKAWA MUASI

(Someone can be seen as a very religious but in reality he/she is rebellious)

 

Nawaambieni ya kwamba mtu anaweza kuonekana mwana dini mzuri sana lakini nawaambia anaweza akawa kwangu ni mwasi. Nasema wafikirieni Mafarisayo, nasema walikuwa wana dini sana lakini nawaambia walikuwa waasi kwangu. Nawaambieni msidanganywe na dini wala msichukuliwe katika mtego wake.

 

 Lakini nawaambieni nitiini Mimi kwani nawaambieni katika utii kuna uzima. Nasema sio katika kutofikiri dini au matendo ya dini, lakini nasema katika kunitii Mimi kuna uzima. Nasema watu wengi watajivisha nyuso za kidini, ili waonekane na watu ili wasifiwe au kupigiwa makofi na watu, ili watu wengine wawanene vizuri.

 

Lakini nawaambia dini sio utii. Nawaambieni nataka watu watiifu, nasema wengi walio wa kidini sana, nasema wao ni waasi wakubwa, nasema wana mioyo migumu kunielekea Mimi. Nasema jifunze Neno langu uone kama sio la kweli, wengi walio wa kidini sana mioyoni mwao ni waasi.

 

 

MUNGU HAHESHIMU DINI

(God does not respect religion)

 

Nasema Mimi Bwana Mungu wenu siheshimu dini, nasema siheshimu dini kwani wengi wataivaa kama kinyago. Nasema wataivaa kama vazi la kujifanya, nasema wataivaa kama joho ili lifunike giza lao; lifunike uovu wao, lifunike hali yao ya dhambi.

 

Nasema Mimi Bwana Mungu wenu siheshimu dini bali nitaikatilia mbali kutoka kwa mwanadamu na nitamfunua katika hali yake ya utupu ili kwamba apate kutubu na kunirudia Mimi.

 

Nawaambieni watu wangu wakati ninapowaambia kuilenga dini nasema ni kwa sababu Mimi siiheshimu dini. Nasema Mimi Bwana . Mungu wenu siwezi kupigia magoti majoho ya dini ya wanadamuLakini nasema nitawakatilia mbali kutoka kwao na kuwafunua katika utupu wao. Nasema nafanya hivyo ili wanadamu wa aibishwe ili wanipigie magoti Mimi Mungu niliye hai.

 

HAKI HAIPATIKANI KATIKA DINI

(No righteousness in religion)

 

Nawaambieni kwamba haki haipatikani katika dini, nasema haki inayotokana na Mimi, nasema haipatikani kwenye dini, kwani nasema haki ya dini ni ya kinafiki, nasema ni ya kimzahamzaha. Nasema hiyo sio haki yangu kabisa.

 

 Nawaambieni haki yangu inapatikana katika utii. Nasema utakaponitii, nasema utafungamana na haki.Nasema utakaponitii Mimi utafungamana na haki nasema nitawapeleka mbele katika utakatifu.

 

KAZI YA ROHO WA MUNGU KWA MWANADAMU

(The work of the Spirit of God in a human being. Issue 35 WOS 1992 pg 11)

 

Nawaambieni kwamba Roho wangu hulia , nasema Roho wangu huita, nasema Roho wangu huita mpaka kwenye kina cha wanadamu, nasema hulia, huita. Nasema huita hadi kwenye kina cha wanadamu.

 

Nasema nawaita watoke nasema yule atakayekuwa wangu, nasema nawaita wao hata sasa hivi, nawaambieni msikate tamaa kwa kazi ya Roho wangu ni tofauti kuliko kazi ya wanadamu. Nasema kazi ya Roho wangu ni ya kina kirefu sana, nasema huita hadi kwenye kina cha mwanadamu, nawaambieni kwamba wanadamu watajijengea ujinga na watauonyesha lakini nawaambieni sio mguso wa kiroho.

 

Roho wangu tu ndio anayeweza kugusa kina cha mtu, nasema Roho wangu tu ndiye awezaye kwenda mpaka kwenye kina kirefu sana cha mtu na kumwita atoke huko, nasema na kumwita atoke huko, nasema na kumkomboa kutoka dhambi, nasema watu wengi watapata udini lakini nasema hawataweza kuguswa na Roho wangu. Nawaambieni kazi ya Roho ni ya ndani sana.

 

Ni kazi inayoingia hata kwenye kina kirefu sana cha mtu. Nasema mruhusu Roho wangu aigie hadi kwenye kina chako, nasema mruhusu awalilie wengine kupitia wewe, kwani nasema Roho wangu anatembea kupitia watu wangu kwani anawaita kwa utulivu nasema nishukuruni kwa Roho wangu.

 

OMBA KAMA ROHO ANAVYOKUONGOZA

(Pray as lead by the Spirit. Issue 35 WOS 1992 Pg. 14)

 

Ningewaambieni ombeni kama Roho wangu anavyowaongoza, omba kama Roho wangu anavyowaelekeza. Lakini nawaambieni wakati Roho wangu anapokuwa hawaongozi na hapo mnafanya tu matendo ya kidini.

 

Kwani nawaambieni mimi Bwana Mungu wenu nazungumza nanyi na kuwaambia ombea hili na hili. Nasema kwahiyo ombea. Lakini nawaambia msiombe maonbi ya kuwafanya muonekane na wanadamu na kusikiwa na wanadamu.

 

Kwani nawaambieni wengi wana mawazo potofu kuhusu kile wanachotakiwa kuombea. Nasema mtii Roho wangu kwani nasema utaomba kama Roho wangu atakavyo amuru. Nasema nitawasikieni. Nasema nitawajibu, lakini nasema wakati mtakapoomba ili mwonekane na watu, nasema maombi yenu yataangukia patupu.

 

 Nasema nitafutieni uso kama ninavyowaongoza, nasema ombeni kama ninavyowaelekeza nasema nitawajibu, nasema nishukuruni mimi kwamba mimi Bwana Mungu wenu ambayo huwajibu maombi yenu.

 

 

WAKATI MWANADAMU ANAPOKUWA KWENYE STAREHE ANASTAWISHA DINI

(When a human being is comfortable he/she establishes religion Issue 16 WOS1990. Pg12)

 

Nawaambieni na ninasema nanyi kwamba wakati watu wangu wanaponifuata Mimi ki ukweli, nasema moto unaambatana nao. Moto unakuwa wao na nasema unachoma kila kilicho kinyume nami. Nawaambieni usiku wa leo msijute kwa msukumo ambao Mimi Bwana Mungu wenu nimeuweka nyie ndani yake.

 

Kwani nawaamba jinsi mtakavyolilia kuniabudu Mimi katika Roho na kweli na Mimi Bwana Mungu wenu naweka msukumo kwenu, ili muweze kuniabudu kiuhalisi katika Roho na kweli. Kwani nawaambieni kwamba wakati watu wanapokuwa wamestarehe wanajaribu kustawisha dini. Na ningewaambia kwamba sitamani kwamba mustawishe dini.

 

Lakini nawaambieni ya kwamba mngebakia moto kwangu, kwani nawaambieni nimewaita ili muwe moto wa kuchoma, ndio nimewaita ili muweze kuchoma. Na nawaambieni kwamba hamwezi kuchoma, kama mko na shughuli nyingi kustawisha dini zenu wenyewe, kwa matengenezo ya watu ya kidini.

 

Nawaambieni ni msukumo unaowafanya watu wangu kunililia. Nasema wengi wanakuja na wengi wanakwenda lakini si wengi wanaoniabudu kikweli, si wengi wanaonitafuta kwa kweli. Nasema ni msukumo unaowaendesha kuja kwangu.

 

 Nasema iweni watu wa shukrani kwa hilo, kwani nasema wakati mwanadamu anamsukumo katika maisha yake kwa ajili yangu, nasema wamebarikiwa .

 Nasema niko pale kukutana nao niko pale kuwaonyesha iliyo kweli na kuwafundisha kweli na kuwaonyesha Roho wangu. Nawaambieni furahini katika hilo.

 

MWANADAMU ANAPOJIJENGEA DHEHEBU LAKE ANADHANI AMESHAFIKA (When a man establishes his religion he thinks he has arrived. Issue 24 WOS. pg 16)

 

Nawaambieni wakati wanadamu wanapojijengea ufalme wao, wakati wanapojiundia madhehebu yao, wananenepa, na wanajitosheleza na wanajituna na wanadhani wamekwisha fika. Nasema hawajafika, kitu walichofanya ni kujihukumia kifo chao wenyewe.

 

Lakini nakuambia wewe kwamba sipendi kwamba ungejihukumia kifo chako mwenyewe bali uzima wako. Nasema simama wazi kwangu, usijinenepeshe na kuwa mvivu na kufanikiwa katika matakwa yako mwenyewe lakini nakuambia wewe kaa ukiwa umepiga magoti mbele zangu, jinyenyekeze.

 

MATEKA NA VIFUNGO KWA SABABU YA DHAMBI

(Captive and in bondage because of sin)

 

Ninawaambieni ninyi siku hii nitawapeni ninyi ufahamu. Ninasema watu wangu nyakati zilizopita hawakuletwa kwenye mateka na kwenye vifungo kwa sababu ya dhambi zao? Na kwa sababu ya uasi wao kwangu?

Ndio nasema mara nyingi hii imetokea kwao. Na wakati wamekuwa katika minyororo mikali mara nyingi wamenililia Mimi na Mimi katika rehema zangu nimeshuka chini na kuwafikia.

 Nasema usifikiri ni kitu kigeni ambacho kimeangusha kanisa katika saa hii, kwa maana ningesema limechukuliwa mateka na katika vifungo kwa sababu ya dhambi zao na uasi wao.

 

Na ningesema nitaruhusu minyororo yao iwe ya majonzi juu yao. Na nitaruhusu vifungo kuwa vikali juu yao. Na nitawaruhusu wao kufahamu kwamba nini maana ya kuwa mtumwa wa dhambi.

 

Kwa maana ninazungumza nanyi na ningependa kuwaambia kwamba wakati watu wangu wanapotamani kitu fulani kingine kuliko Mimi hicho nitawapa wao na kujaa. Na nitazidi kukimiminia kwao, watajiviringisha katika hicho ambacho wamekitamani na wataliwa na hicho ambacho wamekitamania.

 

Kwa maana ningependa kuzungumza nanyi na kusema kwamba Mimi ni Mungu mwenye wivu, na ningependa kusema kwamba wakati mioyo ya watu wangu inapokwenda mbali na Mimi kwamba ninawapa wao kile ambacho wanakitaka na baadae nawaangamiza nacho.Na baadae ninawaruhusu wao waone mateso ya uchguzi wao.

 Lakini nasema nanyi na ninawaambieni kwamba ninainua kiwango cha haki na bendera ya haki saa hii, na ninawaleta watu watakatifu na ninawaleta watu ambao mioyo yao iko safi.

 

Kwa hiyo ninawaambieni msifadhaike wakati mtakapoona utumwa wa wale walio chagua kutamani kwa maana ninasema kwamba wanapata kile ambacho wanakitaka. Ninawaambieni nitakeni Mimi kwa mioyo yenu yote nami nitajimimina mwenyewe juu yenu na nitawafanyeni niyi watumwa wangu, nitawafanyeni ninyi mateka wangu na nitawafanya ninyi watumishi wangu.

 

Lakini mtafurahi katika vitu hivyo kwa sababu vifungo wa vita kuwa vizito wala havitakuwa majonzi. Lakini minyororo itakuwa furaha na amani na milele kwa njia ya Mimi. Ndiyo ninawaambieni ninyi kwamba kuna mistari miwili ya upinzani inayofahamika katika saa hii na inaiona hiyo mbele ya macho yako.

 

Usiwe na majonzi ndiyo usiwe na majonzi lakini afadhali ufahamu kwamba watu wangu wana kijalizia kikombe chao. Kwa maana ninawaambieni kwamba wanapata kile ambacho wamekiomba. Kwa sababu hiyo angalia sana kile unachokiomba fikiri kile ambacho unakitamani na ninatamani Mimi nami nitakujaza.

                                                                                                               Soma Isaya 9.

 

SIKUWARUHUSU NINYI KUPENDEZA MBELE YA MACHO YA WATU

(I did not allow you to please people)

 

Mbali na hapo ninawaambieni hakikisheni nasema hakikisheni yale ambayo ninafanya na hakikisheni idadi yenu na hakikisheni jinsi mlivyo na jinsi msivyo, na angalieni vizuri naman Mimi Bwana Mungu wenu nilivyofanya na ninavyofanya katika ulimwengu huu kupitia ninyi.

 

Kwa maana ningependa kuzungumza nanyi na ningependa kusema kwamba kwa jinsi mtakavyo hakikisha na kama mtakavyo tazama mtaona kwmba ni kazi kubwa ambayo Mimi Bwana Mungu wenu ninaifanya.

 

Na ningependa kuzungumza nanyi na nimesema na ninyi kwamba ni lazima mtambue kwamba ni nguvu yangu na kwamba ni uwezo wangu na kwamba ni utukufu wangu ambao unagusa na ambao unabadilisha na ambao unageuza maisha. Kwa maana ninazungumza na ninyi na ningependa kusema nanyi kwamba Mimi Bwana Mungu wenu ningepokea utukufu kwa maana nimewafanya mpungue chini.

 

Sikuwaruhusu kustawi ili kwamba mseme kwamba ni kwa sababu ya idadi yenu. Sikuwaruhusu muwe matajiri ili kwamba mseme ni kwa sababu ya mali zenu. Sikuwaruhu ninyi kupendeza mbele ya macho ya watu, ili kwamba mseme kwamba ni kwa sababu watu wanawakubali ninyi.

 

 Lakini ninazungumza na ninyi na ninasema kwamba Mimi Bwana Mungu wenu niwatiaye nguvu. Ni Mimi Bwana Mungu wenu ambaye nimetoa uweza wangu juu yako kwa hiyo nasema na ninyi na nina waamuru nanyi kuhakikisha, hakikisheni na muone ambayo Mimi Bwana Mungu wenu ninayoyafanya.

 

HAIJALISHI UNAONEKANA WA KIDINI NAMNA GANI UNAVYOPIGIAMAGOTI NI KIFO NA UHARIBIFU

(I do not care if you look religious. All you are bowing to is death and destruction)

 

Nasema kwamba Mimi ni Mungu aliye hai ambaye huishi katikati ya watu wangu. Nasema sipendi watu wangu watafute miungu mingine lakini kwamba wangenitafuta Mimi. Kwa maana nasema Mimi naishi katikati ya watu wangu.

 

Nasema sipendi kwamba watu wangu waweke macho yao sana juu ya watu wa mataifa, na wajitawale miungu yao. Lakini nasema ninapenda kwamba watu wangu waniangalie.

 

 Kwa maana ninasema kwamba nimekusudia kwamba watu wangu wangenitumikia kwamba wangenifuata kwamba wangenitii kwa maana Mimi ni Mungu aliye hai.

 

Nasema unapokuwa ndani yangu wewe uhai, utakapo tumikia miungu mingine wewe umekufa. Nasema kuna wengi ambao hulipa dhabihu zao za dini hulipa , na kulipa na huwalipa siku nzima. Lakini nasema kwamba hulipa dhabihu zao kwenye kifo. Kwa maana nasema kwamba miungu yao imekufa.

 

Nasema utakapopiga magoti chini na kuniabudu Mimi, nasema upo katika uzima, kwa maana Mimi ni Mungu aliye hai na hutoa vitu vyangu kwako, na hutoa nguvu zangu kwako. Nasema wale ambao wataniabudu Mimi katika Roho na kweli wataishi. Nasema dunia imejaa wafu wanaoishi, watu ambao wako hai katika mwili bali wamekufa katika roho.

 

Nasema wala msishiriki uovu wao wala upotofu wao, wala msishiriki ibada yao ya sanamu lakini nasema nishirikini Mimi kwa maana nasema peke yangu Mimi ni Mungu aliye hai, nasema sipendi kwamba ningekuwa katikati ya wafu.

 

Lakini mngependa kuomba, ningekuwa katikati ya walio hai. Nasema ishi ndani yangu kwa maana Mimi ni Mungu aliye hai. Nasema hakuna tumaini katika miungu mingine kwa maana kuna tumaini gani katika kifo? Nasema hakuna.

 

Nasema wakati wanadamu watakapo pigia magoti vivuli na wanadamu watakapopigia magoti sanamu na katika hili na katika ile nasema wanpigia magoti utupu, kwa maana nasema mwishoni watavuna maangamizo.

 

Nasema mwishoni watavuna uharibifu, nasema hawatavuna uzima. Kwa maana naona hawakupanda katika uzima, lakini wamepanda katika kifo. Nasema haijulishi wanaweza kuonekana wa kidini namna gani nasema wanavyovipigia magoti nasema ni bure.

 

Kwa maana nasema kwamba wanapigia magoti kifo na uharibifu. Nasema hawapigii magoti uzima. Nasema wakati unapopigia magoti unapigia uzima, na nakupa wewe uzima. Nasema nishukuruni Mimi kwa maana ni uzima.

 

WALA MSIISHI KATIKA MAWAZO YA KIDINI

(Do not live in religious thoughts)

 

Nasema wala msiishi katika mawazo ya kidini kama ubora wenu. Lakini nasema muishi katikka nuru . Ruhusuni nuru iwapenyeze ninyi, ruhusuni nuru iwafunue ninyi. Nasema ishini katika nuru. wala msijifunike wenyewe katika blanketi la kujifanya,lakini nasema ruhusuni nuru yangu iwafunike, kwa maana nasema katika nuru yangu kuna uzima, nasema ruhusuni nuru yangu iwafunike.

 

Nasema unaweza kujidanganya mwenyewe lakini Mimi Bwana Mungu wako sidanganyiki kwa maana nakufahamu wewe ni nani na wewe ni nini, na nina fahamu unaishi wapi. Nasema wakati unapokuja safi pamoja na Mimi ndipo mzigo wako unapo nyanyuliwa juu yako lakini nasema wakati unapo jaribu kujifunika mwenyewe nasema unjifunika ukichaa.

 

 Nasema huwezi kujificha mwenyewe kutoka kwangu. Nasema unapokuja safi mzigo unaondolewa, nasema jitoe mwenyewe kwangu na niruhusu mimi Bwana Mungu wako ninyanyue mzigo juu yako na kukutakasa wewe. Nasema nishukuru mimi kwamba mimi ni Mungu wako na muumbaji wako na kwamba ni mfalme na chanzo mkombozi wako.

 

Nishukuru kwa maana sio mwingine ambaye ungeweza kumtegemea bali ni mimi Mungu aliye hai. Nasema nishukuruni mimi kwa maana nuru yangu huja juu yako na kukujia wewe mfululizo.Nishukuruni mimitena kwa maana ni Mungu aliye hai na ninaishi katikati yenu kabisa.

 

Nasema siku hi ya leo shuhuda zenu ruhusuni ziwe za uzima wangu kwa maana mbali na mimi hakuna uzima. Nasema shuhudieni na muwe na furaha kwa maana mimi ni uzima, na ninajitoamwenyewe kwenu nasema nishukuruni mimi maana mimi ni Mungu aliye hai na ninaishi katikati yenu. Nasema nishukuruni mimi kwa maana mimi ni uzima.

 

MAZINGIRA NDIO UZIMA AU MIMI?

(Is circumstance life or Me?)

 

Ningependa nikuulize wewe je, mazingira ndiyo uzima wako au Mimi ndiyo uzima? Nasema furahini na mnishukuru Mimi watu wangu kwa maana Mimi ni uzima. Sio mazingira ambayo yanawapeni ninyi uzima, kwa maana ningependa kuwaambieni kwamba mtu anaweza kujenga kanisa na madirisha yanaweza kuwa makamilifu na mimea inaweza ikaning’inia chini na zulia chini laweza kuwa nene, lakini nauliza je, hayo ni uzima?

 

Ninawaambieni ninyi vitu vinaweza kuwa vya starehe sana, na muziki waweza kuwa laini, lakini nauliza huo ndio uzima? Hapana huo sio uzima. Mimi Bwana Mungu wenu ndiyo uzima.

 

Nasema ninaweza kukutana na watu wangu popote pale watakaponifuata Mimi. Kwa maana ninawaambieni ninyi kwamba wakati ninapo waambia watu wangu hili na hili na wakanitii Mimi, Nasema Mimi Bwana Mungu wenu nitakutana na watu wangu, nasema nishukuruni. Na nasema nishukuruni Mimi sasa kwa kutoa ushuhuda mzito, ndiyo toeni ushuhuda wa nguvu katika ukweli kwamba Mimi ni uzima.

 

WATU WA DINI SIO WA KIROHO BALI NI WA KIMWILI

(Religious people are not Spiritual but carnal)

 

Ninawaambieni ninyi kwamba wanadamu wanapotafuta mipango yao ya usalama wao na kuta za dini zao wenyewe ninawaambieni kwamba sio wa kiroho bali ni wa kimwili.

 

Nasema sipendi watu wa kimwili. Ninapenda watu ambao watakuwa na kiu kwa vitu vya rohoni, ambao watakuwa na kiu na Mimi, ambao watakuwa na njaa na Mimi, ambao watanifuata. Ninawaambieni ninyi kwamba ninaweza kukutana nanyi chini ya mti, nasema ninaweza kukutana na ninyi chumbani, nasema ninaweza kukutana na ninyi popote Roho yangu inapokaa.

 

Kwa maana ninawaambieni ninyi kwamba Mimi Bwana Mungu wenu siwekewi mipaka na kuta za mwanadamu au mipango ya mwanadmu wala dini ya mwanadamu.

 

Ninawaambieni ninyi tafuteni kufuata Roho, msitafute kubakia katika ulimwengu wa kimwili bali tafuteni kuja katika Roho. Kwa maana nawaambieni ninyi kwamba katika Roho ni uzima lakini katika mwili ni kifo.

 

KATIKA DINI MWILI HUIGIZA ROHO

(In religion, flesh imitates the Spirit)

  

Ninawaambieni ninyi kwamba katika dini ni kwamba mwili huijaza roho, lakini nasema kwamba hakika Mimi Bwana Mungu wenu ninafahamu tofauti. Ninasema kwamba kile ambacho kimeigizwa hakikubaliki kwangu. Ninasema ni dhabihu ya uwongo na ninasema nitaitupilia mbali. Nasema ni harufu mbaya katika pua zangu.

 

Nasema usiangukie kwenye mawindo ya dhabihu za uwongo lakini nitoleeni Mimi sadaka ya kweli, ndiyo nitoleeni Mimi sadaka ya kweli.

 

 Kwa maana kwamba vitu hivyo vinakubalika kwangu. Ndiyo, vitu hivyo huja mbele zangu na vinapendeza kwangu. Nasema Mimi Bwana Mungu wenu ni Roho, nasema nitakubali yale ambayo ni Roho.

 

 

WENGINE WA KIDINI WA HALI YA JUU

(Others are highly religious)

 

Nasema katika siku hizi ni kwamba nitamimina vitu vyangu juu ya wale ambao watavipokea, juu ya wale ambao watavipokea kwa shukrani kubwa. Nasema wengi ni wa dini wa hali ya juu, na hawatapokea vitu ambavyo nitavimimina, lakini nasema kwamba Mimi Bwana Mungu wako nitavimimina tu.

 

Ninawaambieni wakati watakapokuwa wazi kwangu nitapokea, nasema wakati mtakapokunja magotini nitapokea. Mara kwa mara pigeni magoti mbele zangu na mpokee vile ambavyo nimeviandaa. Kwa maana nasema kweli Mimi ni Mungu aliye hai ambaye huishi katikati ya watu wake. Nasema kwamba nitajimimina mwenyewe juu ya wale ambao watapokea.

 

INUKA UANGAZE

(Rise and shine!)

 

Watoto wangu nasema nanyi siku hii ya leo na ninawapa hekima hii ambayo hamkuwa nayo nyakati zilizopita. Ninawaabieni, kama mkiangalia nyuma katika enzi zilizopita za kanisa mngeona kwamba kanisa limejisukuma lenyewe chini katika giza kuu.

 

 Kama hawakuwa wachache wanyenyekevu ambao walinitafuta uso kwa karne nyingi, kweli yangu ingekuwa imekwisha potea. Lakini mara zote kumekuwepo na wale ambao hunitafuta, na wale ambao wame nitafuta Mimi kwa mioyo yao yote. Katika siku hii ya leo na saa hii kanisa limefikia katika hali ya kujadiliana na dunia kiasi kwamba limetoa nguvu zake katika dunia. Lakini ndiyo nasema hakuna nguvu iliyobaki katika kanisa langu. Lakini kuna wachache hapa na wachache pale ambao wananitafuta uso wangu.

 

Duniani kote, nina wainua wale ambao wamenitafuta katika unyenyekevu wote na kweli. Usitafute kukubaliwa na kanisa la kidini kwa maana hautapata. Kwa sababu nina kuongoza mbele na kukuongoza katika njia iliyo wazi na katika nuru yangu. Lakini utakuja kinyume na giza nene lakini lile giza nene litakuwa udanganyifu kwa wanadamu, kwa sababu mwanadamu amelichagua dhidi yangu.

 

Lakini ninakupa wewe uchaguzi kati ya starehe na majadiliano, kati ya kweli yangu na neno langu kwa sababu nuru yangu huangaza kwenye giza na wewe utaona zaidi na zaidi vitu vinavyoendelea katika giza.

 

Ninapokupa nuru zaidi utaona zaidi yanayoendelea katika giza la majadiliano. Ndiyo, itakushtua na kukushangaza lakini nasema ni lazima uendelee kutembea katika nuru niliyokupa.Nitakupa uchaguzi katika kila hatua ya njia na kama uatatafuta kunijia Mimi na kunichagua ndiyo, nasema kwamba utaendelea katika nuru kubwa na nitaleta vingi kutoka kwako. Ninahitaji kwamba uyatoe maisha yako na ninahitaji kwamba uendelee kunifahamu Mimi na hatua ambazo nilizitembea katika uso wa dunia hii.

 

Hii sio mchezo bali vita. Nimekuita wewe uendelee mbele usiangalie nyuma au kupiga kambi ya majadiliano au kunyamazishwa na usalama wa dunia au kanisa la kidunia na giza ambapo lipo hapa kwa sababu nitalifunua na wewe utashtushwa. Je, utanifuata? Mimi ni kamanda wako Mkuu na ni lazima utembee mbele katika amri nyuma yangu kwa sababu nina iongoza vita hii.

 

OMBOLEZA KWA AJILI YA WATU WANGU

(Weep for my people)

 

Nasema na ninyi siku hii ya leo na ningependa kuwaambieni kwamba wakati utakapoona maneno ya machukizo yameenea, na wakati mtakapoona uharibifu umejaa, nasema ombolezeni kwa ajili ya watu wangu kwa maana nawaambieni ninyi kwamba nani atawaongoza kondoo wangu?

 

Nani atawaelekeza kondoo wangu? Ni nani atakayewaleta watu wangu katika kweli na katika haki, nani atakayewasaidia kuona kosa la njia zao? Nasema, hakuna. Nasema hakuna anayenihubiri Mimi kama nilivyo, na hiyo ina waacha wapi watu wangu, lakini kuzurura kwa upofu na kuwafata viongozi vipofu.

 

Ninawaambieni ninyi kwamba ombolezeni kwa ajili ya watu wangu, kwamba waweze kuja chini ya viongozi ambao watawaongoza ili waweze kuja katika nuru ili wasije wakakwama kwenye dimbwi lakini waweze kutembea katika nuru iliyonyooka.

 

Kwa maana ninawaambieni kwamba wale ambao wanatangaza kuwa ni wangu wana muda mrefu tangu niondoke na nasema kwamba watu wangu ndiyo wahusika.

 

KULAANIWA NA KUNYAUKA KWA MAKANISA

(Cursed and weathered churches)

 

Ningependa kuzungumza na kusema kwamba Mimi Bwana Mungu wenu nililaani na kunyausha mti usiozaa matunda. Hivyo nimelaani na kunyausha makanisa katika sehemu hii, kwa sababu hayazai matunda.

 

Lakini ningependa kusema kwamba Mimi Bwana Mungu wenu nimekupeni ninyi uhai. Nimewabarikieni ninyi na uzima, msiaibike mnapoendelea mbele katika uzima wangu. Msione aibu lakini nasema fahamuni kwamba mna uzima kwa maana nimewapeni ninyi, na wengine wamenyauka.

 

USITAFUTE KUMFURAHISHA MTU WA DINI

(Don’t seek to please religious people)

 

Nasema nanyi siku hii ya leo na nigependa kuwaambia kwamba hakuna mtu anyenifahamu. Ndiyo, hakuna mtu anyenifahamu na anyeweza kunichambua na kuniunda na kuweza kunichunguza. Kwa maana nawaambieni kwamba Mimi ni Mungu. Nawaambieni Mimi ni Muumbaji wa mbingu na nchi na nilikufanya na usingeweza kujifanya hivyo mwenyewe.

 

Nawaambieni msijaribu kunichunguza na kunichambua bali nifuateni na jitoeni kwangu. Kwa vitu ambavyo ninavifanya. Kama vitu ambavyo ninavileta pamoja, vitu ambavyo ningefanya, ni vya ajabu sana vilivyokwisha kufanywa kutokana na shauri langu mwenyewe.

 

Na ningependa niwaambieni kwamba kuna vitu ambavyo hutaweza kuvielewa haijalishi ni kiasi gani unavyokaza akili yako. Nawaambieni ninyi msikaze sana akili zenu bali niaminini Mimi, na ufahamu kuwa Mimi Bwana Mungu wenu nitafanya vitu hivyo ambavyo vipo katika moyo wangu, na ufahamu ya kuwa Mimi Bwana Mungu wenu nitatuma watu watakaojizamisha kwangu.

 

Zaidi sana nawaambieni ninyi msiangalie mazingira mliyonayo, na usijaribu kujilinganisha wewe na wale wanaokuzunguka kwa maana nawaambieni kwamba nimewaita kuwa watu ambao sio wa kawaida.

 

Na nikaweka mhuri wangu juu yenu, na ninasema wale ambao ni wa kipekee hawatafaa ulimwenguni. Hawatafaa katika babeli ya dini, lakini watafaa kwangu kwa maana vile ndivyo ilivyomaanishwa kufanya ni kunitosheleza Mimi. Usitafute kuridhisha ulimwengu, usitafute kumridhisha mtu wa dini bali tafuta kuniridhisha Mimi maana ndilo kusudi ambalo nilikuambia wewe na vile vile nimekuleta na kuweka alama yangu juu yako.

 

UCHAJI WA DINI

(Fear of religion)

 

Nasema kuwa maisha yangu ni kama mto unaooendelea. Nasema unakutiririkia, nasema unakutiririkia ili kukuosha wewe, kukutakasa wewe, kukufanya wewe uwe safi, nasema kukutuliza kiu yako. Nasema uwe unafurahi kwa ajili ya maji yangu. Nasema uwe na tumbo kwa ajili ya mto wangu kwa maana nasema ndio uzima.

 

Nawaambieni kwamba kila mtu nasema anatafuta mto wa uzima. Nasema hutafuta njia ya kujitakasa wenyewe. Nasema wengi wamejengwa juu ya uchaji wao wa dini.

 

Lakini nawaambieni ninyi kwamba hawataweza kujitakasa wenyewe kwa maana nawaambieni kwamba kuna njia moja tu ya kuweza kufanywa safi nayo ni kwa Mimi. Nasema tu kupittia katika maji yangu ndipo mtu atakapoweza kufanywa safi.

 

 Nasema sio kwa njia ya mito ya asili ya ulimwengu bali nasema katika mito ya Roho wangu. Nasema watu wangu furahini kwamba maji huwa yanatiririka kwenu ili kuwafanyeni safi, ili kuwafanya weupe, kwamba yatakase fahamu zenu, yatakase miili yenu, yatakase mioyo yenu.

 

TUPA DINI YAKO PEMBENI

(Put your religion aside)

 

Nawaambieni ninyi watu wangu ni wakipekee na nasema kwamba nitawatumia kama ninavyopenda Mimi. Je, tatizo liko wapi namna nitakavyo kutumia? Kwa maana nasema wakati utakapokuwa wa dini, nasema utaniwekea mipaka. Lakini nasema wakati utakapotupa dini yako pembeni nasema ndipo utakapoona utukufu wangu.

 

Nawaambieni ninyi watu wangu msifadhaike wenyewe jinsi nitakavyowachagua kuwatumia. Kwa maana nasema ninyi ni mali yangu, nasema ninyi ni watu wangu wa kipekee. Nasema je, siwezi nikawatumia Mimi kwa namna ya kipekee? Nasema kwa namna ambayo inanipendeza Mimi.?

 

Nasema furahini, nasema furahini kwa maana Mimi ni Mungu wenu, kwa maana Mimi ni muumbaji wenu, nasema furahini kwa maana natawala katika mamlaka kubwa kuliko zote juu yenu. Nasema watu katika udini wao wote wamenikosea sana , kwa maana wamejiweka katika hali ya kudumaa, nasema wamejiweka katika hali ya uovu, nasema wamejiweka katika hali ya ubaya na bado wanasema ni Mimi.

Nasema ni uongo, nasema usijiwekee vitu hivyo lakini nasema tembea nami kwa maana Mimi ni Mungu wako.

 

HAMU YA MUNGU KUSHIRIKIANA NA WANADAMU

(God desires to fellowship with His people)

 

Nasema imekuwa ni hamu yangu kushirikiana na watu wangu lakini watu wangu hakuna hata mmoja anayenipata mimi. Nasema wamechagua taratibu za kidunia . Nasema wamechagua kuchanganyikiwa kwa dini. Nasema wamechagua gereza nyumba ya dhambi. Lakini nasema ilikuwa hamu yangu kushirikiana na watu wangu. Nasema msinikanyage yangu kwa watu wangu.

 

Nasema natamani kuwaheshimukwa urithi wangu. Nasema natamani kuwaheshimu kwa urithi wangu, nasema kwangu msinikanyage, nasema msinikatishe tamaa lakini nasema nipeni kile ninachokipenda kwani nawaambia nitapendelea ndani yenu. kama uzi chini ya miguu yenu, nasema msinikatishe tamaa lakini nasema bakieni kwangu.

 

Nasema bakieni kwenye ushirika nami kwani nasema hivyo ndivyo ninavyopenda hiyo ndiyo hamu yangu. Kwani natamani kujimimina nafsi yangu kwa wapendwa wangu.

 

 

MUNGU NI UZIMA MSIFUNGIWE KWENYE MAONYESHO YA KIDINI

(God is life. Do not be locked in religious shows)

 

Ningeongea siku ya leo na kuwaulizeni je, Mimi Bwana Mungu wenu si uzima? Je, Mimi Bwana Mungu wenu sio uhai ? Je, si Mimi Bwana Mungu wenu niletaye uzima kati yenu? Nawaambia je, mta waangalia wanadamu au mtaniangalia Mimi? Kwani nawaambia wakati mtakapo waangalia wanadamu mtakuwa mmeshushwa chini lakini nawaambia wakati mtakaponiangalia Mimi mtakua kwenye uzima.

 

Kwani nawaambieni Mimi ndimi uzima. Ningewaambieni siku ya leo msifungiwe kwenye maonyesho ya kidini, msifungiwe kwemye shughuli na maonyesho ya kidini kwani nasema ni ya kipumbavu, nasema kwamba ni ya kibatili si kitu chenye heshima katika macho yangu. Nawaambieni hayo ni maovu na machukizo, nasema wanatenda matendo maovu bado wanasema ni wangu. Nasema wakati mtakapofingiwa kwenye maonyesho yao, nasema wakati mtakapofungwa na majigambo yao na majivuno yao, nasema manaangalia kitu kisicho heshimika. Nasema wao ni chukizo, nasema wao sio safi, nasema Mimi sio mwenzao, Mimi sio Bwana wao lakini nasema watajiwekea na kujifanyia kila kitu na waseme ni Roho wangu, nasema watasema ni neno langu. Oh! watasema ni kweli yangu, watasema ni utawala wangu lakini nasema ni waongo; nasema ni waovu.

 

Nasema watajionyesha wenyewe wazi wazi katika kila kitu ambacho kitawatazama, katika kila kitu ambacho kitawapa, katika kila kitu ambacho kitajikusudia chenyewe kwao. Nasema wako kama makahaba, wanajiachilia wenyewe, nasema kwa nini unaangalia uovu wao?.

Nasema kwanini unaangalia uovu wao na hatimaye unauleta juu katika uso wangu kama kwamba ningeukubali ? Nakuambia ni chukizo wakati utakapo jilinganisha wewe na wao.

 

Ni nyi sio wenye busara bali ni wapumbavu kwa maana nasema hawapo katika ufalme wangu, bali ni waovu wameharibika ni chukizo. Nasema wanatoa utupu wao na kujiuza, wanaonyesha mapambo yao, wanaonyesha uzuri wao, wanajifunua, lakini nasema wao ni chukizo. Nsema ni waovu.

 

Nasema usijiweke katika maonyesho yao na kusema kwamba yanatoka kwangu kwa maana hayatoki kwangu, nasema ni uovu mbele zangu. Nasema wanadamu wanaweza kujenga kazi kubwa za kidini lakini hata moja sio yangu.

 

Nasema hawatimizi matakwa yangu, lakini nasema wanatimiza mawazo yao maovu,ili kwamba waweze kuwa wafalme katika dunia hii. Nasema usijitaabishe ilikuwa kama walivyo, usijusumbue kuanzisha kazi lakini nasaema kirahisi tu tafuta kunifuta Mimi kwa maana hapo ndipo unapo nitosheleza.

 

Ua kile kiburi ambacho kingejipigilia kwako, ua kile kiburi ambacho kingetafuta kukula na kukanyaga vile vitu vya thamani vinavyotoka katika Roho yangu. Ua kile kiburi ambacho ni mnyama katili anayetafuta sehemu yake mwenyewe kutambulikana mwenyewe utawala wake mwenyewe.

 

Nasema ua hiyo nasema nitafuteni kwa maana nasema Mimi ni uzima. Nasema nishukuruni kwa maneno yangu maana ni uzima, nasema kama maneno yangu yataleta matatizo kwako nasema furahini, kwa maana ndivyo yanavyo maanisha. Kwa maana nawaambieni kwamba hakuna mtu aliyekwisha kufika au kuwa mkamilifu kwa nafsi yake, lakini nasema kwa kupitia Mimi mtu hugeuzwa nishukuruni tena kwamba Mimi ni uzima na kwamba umejaliwa kunishiriki.

 

MIKAKATI YA VITA

(Battle strategies)

 

Mwanangu, ninapenda wewe uwape watu wangu maelekezo haya . Ndiyo ninakuambia wewe kwamba ni lazima uwaeleze watu wangu kwanza kabisa kwamba ni lazima waweke macho yao na mioyo yao ikiwa imekaa juu yangu.

 

Ndiyo, ni lazima uwaeleze kama wakiweka mioyo yao na macho yao yakikaa juu yangu kwamba watatembea kwa umoja.

 

Na ninakueleza zaidi kwamba ni lazima uwaeleze kwamba hawatakiwi kuanagalia kushoto au kuangalia kulia. Bali ni lazima waweke mioyo yao na macho yao yamekaa juu yangu. Lazima wateke nyara fikra zao zitii, ndiyo zitii Roho wangu na mapenzi yangu katika maisha yao. Waambie vile vile kikosi changu kwamba ni lazima watembee katika umoja kama ninavyoongoza. Kwa maana ninaweka amri na kwa jinsi itakavyokuja utaona kwamba imeamrishwa na Mimi.

 

Ndiyo na ni lazima uwaambie kwamba kujitoa kwao ni lazima kujitoa hata kuja. Waambie kwamba nina taka kwamba wangetoa mioyo yao yote na maisha yao kwangu. Kwa maana ninapenda nielekeze kila mwendo ambao wanaufanya. Ninapenda kwamba watafute uso wangu katika kila maamuzi.

 

Zaidi sana waelekeze wao kwamba hii siyo saa ya amani, kwamba sijawaita watu wangu katika saa ya amani, bali nimewaita watu wangu mbele kwa vita. Ni lazima uwaeleze kuwa katika vita wata umizwa, kwamba katika vita watajikuta wana vidonda. Kwamba katika vita kuta kuwepo na adui, kuna adui lakini hiyo katika vita kama wakiweka macho yao, mioyo yao na fahamu zao juu yangu ,kwamba nitaleta kila ushindi.

 

Nina jema zidi ya hapo kwamba hawataweza kuelewa mara zote mikakati ambayo ninaiweka, lakini sijawataka jeshi langu watoto wangu kuelewa, ninawataka watii. Ni lazima zaidi uwaelekeze watu wangu kwamba utii ni muhimu sana ni lazima.

 

1. Ni lazima wawe watiifu katika sauti yangu, ni lazima wawe watiifu katika Roho wangu. Kama nikimpa mojawapo wa wanachama wa jeshi langu hali fulani, au kama nikiwapa wao neno kwamba ni lazima walisema kwa ajili yangu, ni lazima wawe watiifu kulitoa.

 

2. Waambie kwamba ni lazima wawe na amani wao kwa wao kwa sababu jeshi amabalo limegawanyika, jeshi ambalo linasengenyana, jeshi ambalo linakulana haliwezi kusimama dhidi ya adui.

 

3. Waelekeze watu wangu kwamba ni lazima waweke mioyo yao macho yao fahamu zao zikiwa zimeelekezwa kwangu.

 

UTII, AMANI KATI YAO, MIOYO, MACHO, NA FAHAMU, ZIKIWA ZIMEKAA KWANGU, na zaidi ya hapo kwambaWASIJADILIANE katika alama yeyote ambayo nimeiweka.Ni lazima wafunge nyonga zao, wajifunge wenyewe kwa maana siku za vita ziko hapa. Vita vimeanza na maadui wakokila mahali, lakini kama wakikaa ndani ya sanduku la usalama ambalo ninalitoa , kila ushindi utakuwa wao.

 

NI LAZIMA MARA KWA MARA UWE TAYARI KUPIGANA

(You must be able to fight at any time)

 

Nasema ni lazima mara kwa mara uwe tayari kupigana wala usilaze mgongo wako kwenye kiti chako kizuri na kuegesha miguu yako na kupitisha pitisha mkono kwenye tumbo lako. Lakini ni lazima uwe tayari kupigana, nasema uvae silaha ni lazima uwe tayari kufanya vita.

 

Nasema usiegemee kwenye kiti chako kizuri na miguu yako ikiwa ime shikiliwa juu na kupitisha pitisha mikono kwenye tumbo lako, kwa maana ninasema sio wakati wa hayo.

 

Nasema wala haujakuwepo wakati wa hayo kwa watu wangu wa kweli, kwa maana nasema kwamba ndivyo kanisa lilivyojinajisi na kujipeleka lenyewe gerezani kwa maana nasema limejiegemeza lenyewe katika kiti chake kirahisi na limeuza kiti chake kirahisi kwa kitanda cha maji na sasa limegeuka kuwa kahaba.

 

Lakini ninawaambieni ninyi msichukue starehe lakini simameni kwa makini. Kaeni macho, kueni kwenye ulinzi, kwa maana nasema Mimi Bwana Mungu wenu nitamfunua adui kwenu kama mko macho.Kwa maelezo zaidi kuhusu ACMTC TANZANIA, au jinsi utakavyoweza kujihusisha, wasiliana na Meja Frank & Elina Materu: S.L.P. 7579 Dar es Salaam, Tanzania. Barua pepe: materufrank@yahoo.com