Home || The Aggressive Vision || Prophetic Word Of The Lord || On Line Library || Current Articles and What's New
Free Literature || Visions from The Lord || More About ACMTC || Contact 

(Words of the Spirit)


Maneno ya Roho


MANENO YA UNABII, MANENO YA HEKIMA, UFAHAMU, NA MAARIFA WAKATI

ULIOPITA, ULIOPO NA UJAO


Toleo la 2


(Our Daily Bread)

Mkate wetu wa kila Siku

         

BWANA MUNGU WENU NI MTU WA VITA


Ninawaambieni ninyi kwamba mimi Bwana Mungu wenu, ni mtu wa vita na nitachukua mataifa kwa Roho yangu. Na ningependa kuwaambieni ninyi kwamba kwa jinsi mtakavyojitoa kwangu na kwa jinsi mtakavyonitii ni kwamba mtafuatana nami. Naam, mtaniona mimi nikichukua mataifa kwa Roho yangu kwa maana ninazungumza nanyi na ningependa kuwaambieni ninyi kwamba mimi Bwana Mungu wenu ninavyotangaza vita, naam sirudi nyuma katika wito ule, naam ninaendelea mbele ambako tarumbeta imelia.


Naam, kwa maana ninazungumza nanyi na ninawaambieni niyi kwamba mimi Bwana Mungu wenu ni mtu wa vita. Na siogopi vita. Kwa maana ningependa kuwaambieni kwamba wakati ninapokutana na changamoto ya vita nitaonyesha ujasiri wangu na nguvu yangu .Na sishindwi wala sivunjwi moyo, wala situpwi katika dunia hii. Na nitaonyesha nguvu yangu ya Roho kwamba mimi Bwana Mungu wenu, huchukua mataifa.


VITA INAENDELEA, INAHITAJI UJASIRI NA UNYENYEKEVU KUSHINDA


Wajasiri, wajasiri, wajasiri na wanyenyekevu, watu wangu. Vita inaendelea na watu wangu wanapigana katika sehemu tofauti za dunia. Vita inaendelea. Vita kwa ajili ya nafsi za watu. Inatakiwa ujasiri na unyenyekevu kushinda vita vinavyoendelea. Watu wangu wanapigana katika sehemu mbalimbali za dunia. Inawezekana usiwaone, lakini wanapigana.Kwasababu nimeweka ule mori wa kupigana katika mioyo yao. Na ninawaita mbele kupigana. Ninawaita mbele kushinda kwa sababu wao ni watu wangu na ni maono yangu. Na ninataka jeshi na ninawataka washinde. Na inatakiwa ujasiri na unyenyekevu kwa jeshi hilo kushinda.


KUNA PEPO LINALOITWA FELLOWSHIP


Ninazungumza na ninyi siku hii ya leo na ninawaambieni ninyi kwamba kuna pepo hasa katika eneo hili. Nitawatambulisheni hilo kwenu nanyi mtafikiri "ah, hiyo haiwezekani". Lakini ninawaambieni jinsi mtakavyokuja katika uwepo wangu kwamba mimi Bwana Mungu wenu nitatambua kati ya jema na ovu na nitawaambieni ninyi. Nasema kwamba pepo katika eneohili linaitwa fellowship.Na ninasema kwamba ni roho ya uongo na ni roho ya utumwa nayo imeenda sehemi zote katika mwili wangu. Na watu wamewazia kwamba ni lazima wawe na fellowship na fellowship ni roho ya uongo.


Si kwamba hakuna fellowship ya kweli kati ya waamini wa ukweli, lakini ningewaambieni ninyi kwamba wachache sana ni waamini wa kweli. Na fellowship inaambatana na kila aina ya dhambi kila aina ya uovu, kila aina ya udanganyifu na imefungwa katika pepo moja la kitumwa. Na ninawaambieni likemeeni. Liamuruni liwaondokeni. Nawaambieni lilazimisheni liwaondoke ninyi. Kwa maana ninasema kwamba mna fellowship na mimi na mna fellowship mmoja na mwigine. Kama mnafikiri hiyo haitoshi na mnataka kufellowship na pepo fellowship ndipo umedanganyika. Ninawaambieni ninyi siku hii ya leo liamuruni liondoke.


KILA DHEHEBU LIMETAFUTA KUWAPENDEKEZA WANADAMU ZAIDI KULIKO MUNGU


Ninazungumza na ninyi na ningependa kuwaambieni ninyi msitafute kuwapendeza wanadamu. Msitafute ili watu wawakubali na wazungumze vizuri juu yenu. Kwa maana ningependa kusema nanyi kwamba wengi wameondoka kwangu kwa sababu hawakukipenda kikombe cha kutengwa. Kwa sababu hawakukipenda kikombe cha udhia na wakatafuta kuwapendezesha wanadamu na mimi hapo hapo. Ninawaambieni ninyi hiyo haiwezekani. Nasema wanakonda, sio hapa tu bali dunia nzima. Kwa sababu wachungaji wangu hawalilishi kundi, nasema wanakonda kwa njaa.


Na ninasema ninawapeni ninyi mkate ili mkawape, wala msichoke katika kazi ambayo nimewapeni ninyi. Unasema kwamba unataka kufanya kazi kwa ajili yangu, na kwasababu hukupokea utukufu hupendi kazi yangu. Wewe ni mjinga. Kwa maana kama unatamani kuwa mfalme au malkia katika kiti cha enzi, upo mahali ambapo sio pake. Lakini kama unataka kutumikia upo mahali pake.


Kwa maana ninasema kwamba Mimi Bwana Mungu wenu ninawagawieni ninyi kitu changu ili kwamba mkaweze kuwagawia wengine ili mkaweze kufanya kazi pamoja katika jitihada ya ushirikiano.Kuwagawia mkate wa kuwatia nguvu wale wanaokufa. Nasema kama ungeweza kuona katika roho, ungeona umuhimu wa jinsi kazi ilivyo ambayo nimewapeni ninyi. Na ungeona jinsi ulivyo mjinga, uzembe wako wa kitoto ulivyo na hali yako ilivyo unavyo kaa kaa na ungeona aibu.

 

NINYI NI WATU WANGU AGGRESSIVE


Usiogope kwa ajili ya jina aggressive. Usiwe na hofu wala usiliogope. Kwa maana wewe ni silaha yangu ya vita. Na ninyi ni watu wangu shupavu. Na hilo ndio jina langu ambalo mara zote limekuwa hivyo. Na nimewaiteni ninyi katika vita vya kudumu na vita havitasimama. Kwa hiyo wala usirudi nyuma katika hivyo, wala kuogopa lile jina ambalo nimewapeni ninyi- AGGRESSIVE


KUHUSIANA NA MANENO YA ROHO


Ningependa kusema na ninyi maneno ambayo ninawapeni ninyi, nasema ambayo mnayaweka katika MANENO YA ROHO, nasema msiyapunguze maneno hayo. Nasema msiyachezee maneno hayo. lakini ningewaambieni ninyi, kama nitakavyoyatoa maneno haya myatoe hivyo hivyo. Kwa maana ninawaambieni ninyi kwamba matoleo haya yatabadilisha mioyo ya watu. Nasema yatabadilisha nia za watu, sio kwa sababu ni uchapishaji, bali kwa sababu yanatoka kwangu. Nasema kwa sababu ni kweli itawabadilisha watu

 

KUHUSINA NA ACMTC NA VYEO


Nasema wakati nawapeni jina ACMTC na nikawapa vyeo sikuwapeni vitu hivyo kama vitu vya kujionyesha. Naam lakini nilitoa vitu hivyo kuwa kama vyuma vyekundu vyenye moto mkali sana vya kuchoma katika moyo wako. Naam, na vimekuwa hivyo hivyo. Na wale ambao hawakuruhusu vitu hivyo kuchoma katika mioyo yao naam, wamekwenda, wamekwenda. Lakini ninazungumza nanyi na ninasema kwamba nitaendelea kuchomea vitu hivyo katika mioyo yenu.


KUHUSIANA NA MLIO WA VITA


Mimi Bwana Mungu wenu nitaongeza sauti yangu katika dunia hii. Ninawaambieni ninyi kwamba nime wainueni ninyi juu kuwaleteni ninyi mahali ambapo msingeweza kwenda. Je, si Mimi Bwana Mungu wenu niliyefanya jambo hili? Nazungumza na ninyi na ninasema mbakie kuwa waaminifu kwangu na mniombe Mimi niongeza sauti yangu katika dunia hii. Msisifiwe na mtu na wala kujaribiwa kwa majaribu yake, lakini afadhali uwe mwaminifu kwangu.


Kwa maana ninasema nanyi kwamba nitaongeza sauti yangu katika dunia hii. Nitaongeza ujazo na nitaongeza uwezo na nitaongeza eneo ambalo linafika. Kwa maana ningependa kusema nanyi kwamba Mimi Bwana Mungu wenu ninaliza sauti yangu. Ninawatangazia watu wangu ninaliza SAUTI YANGU YA VITA, na ninawaambieni ninyi bakieni waaminifu kwangu. Aminini kila ninachowaambieni ninyi kwa maana nasema Mimi Bwana Mungu wenu nitaongeza sauti yangu.


KUHUSIANA NA HUDUMA YA UPENDO WA BURE

         

Tulichukua jina HUDUMA ZA UPENDO WA BURE katika amri ya Bwana. Wakati wa mwanzoni alipotueleza tutumie jina hilo tulifikiri ni kitu kigeni lakini baada ya kwenda mbele zake na kutafuta hekima zake, alituruhusu kuelewa ya kwamba hafanyi makosa katika yule anayoyafanya, na kwamba alikuwa na sababu nzuri sana kwa kuchagua jina ambalo dunia ingelidhihaki ili akaweze kupitia kuonyesha utukufu wake. Kwanza kabisa upendo wa Mungu kwa mwanadamu ulitolewa bure kwa njia ya kumtoa mwanawe Yesu Kristo.


Hakuna hata mara moja tunaposoma ambapo Mungu anahitaji malipo kutoka kwetu ili kumpokea Mwokozi kwa uwezo wetu. Pili neno linasema "kununua kweli na kutoiuza" Hivyo hii ina maana kwamba inatubidi kununua kweli kwa njia ya kuweka maisha yetu chini mbele ya Bwana na kwamba hatutakiwi kuiuza ile kweli bali kutoa kama Bwana alivyotoa kwa sababu tumepewa bure na tunatoa bure.


Mungu ameturuhusu kufahamu kwamba tumeanzishiwa na Yeye na kwamba katika saa hii ya wahubiri wa choyo, wapora fedha ametuinua kuwa tofauti kwa sababu inabidi tumtumainie Yesu mfano, alikuja akitoa na alitoa yote ili kwamba tukaweze kupata uzima wa milele.


 Sisi basi ni lazima tukumbuke kwamba upendo wake ni bure kuwashirikisha wengine. Hebu tuchochee upendo wa bure tuliopewa na hapo hapo tuutoe tena ili wengine waweze kumfahamu Mwokozi wetu mtukufu. Huduma za upendo wa bure ni nini? Ni upendo wa Mungu unaotolewa saa na saa tena ukisahihisha na kufundisha upendo utakao tufanya askari wenye nguvu wa msalaba.


KUHUSIANA WITO WA TARUMBETA


Naam sauti yangu itakuwa kama tarumbeta, itavuma dunia nzima kama tarumbeta. Naam nitaiinua na itakuwa utisho na itavuma katika masikio ya watu kama tarumbeta, naam naweza kupiga tarumbeta ya sauti yangu na naweza kuifanya ivume mbali na mapana na watu wataisikia nao watakuja katika toba katika wito huo na sauti hiyo ya tarumbeta itawaita katika magoti yao nao watakuja na kunitafuta Mimi.


KUHUSIANA NA OPERESHENI UOKOAJI


Nazungumza nanyi jioni hii na ningependa kusema, msichoke kutoa sauti ya kuashiria. Naam, msichoke bali endeleeni kwa ujasiri. Kwa maana nazungumza nanyi na ninnasema na nanyi kwamba hii ni saa ya kuchanganyikiwa kwingi, na watu wanasikia sauti nyingi, na wala hawana hakika na njia walizoongozwa.


Na ningependa kuwaambieni ninyi msichoke katika kutangaza kweli. Kwa maana ningependa kuwaambieni kwamba, ni mawimbi makubwa yanatembea. Ni mawimbi makubwa yanayokuja. Ni bahari iliyochafuka na watu wanapotea na wanazama katika safina ya usalama. Na nimewapenininyi ishara ya kupiga itoe mlio na nimewapeni ninyi nuru kwamba wakaweze kuiona na kuponyoka na kuokoka.


Ningependa kuzungumza nanyi na kusema msichoke kama hawakukusikia wewe kwa mara ya kwanza namara ya pili au hata mara ya tatu lakini endelea. Kwa maana ninawaambieni ninyi kwamba ni wakati wa kuchanganya sana na bahari inayochanganya ambayo wamenaswa. Ninawaambieni endeleeni mbele kwa ujasiri, endeleeni msiyumbe, endeleeni kurudia kile ambacho ninawapeni, rudia. Na ningependa kuwaambieni ninyi kwamba mabaki yatakuja katika safina na mabaki wataokolewa.


KUHUSIANA NA KUREGESHA HUDUMA


Nazungumza nanyi siku hii ya leo na ninawaambieni ninyi kwamba, Mimi Bwana Mungu wenu napenda kurejesha uamsho. Nasema simama na tafakari uamsho ukoje. Kwa maana nawaambieni ninyi kwamba ni kazi ngumu. Ninawaambieni mnahitaji nguvu. Nasema nanyi kwamba ni maumivu yaliyo shikiliwa na kushikilia kile ambacho ni kizuri ingawaje kimefunikwa na uchafu, ingawaje kimefunikwa na uovu, ingawaje kimefunikwa na unyonge. Na nasema fikiri urejesho una maana gani. Nasema tafakari kazi ambayo ninataka kuileta.


Nasema natamani kurejesha katika watu wangu haki. Natamani kuwarejesha watu wangu kwenye kifua changu tena. Ninawaambieni kurejesha uamsho. Sio kazi rahisi. Nasema ni kazi ya juhudi. Nasema ni kazi ya upendo, nasema ni kazi ya juhudi nyingi. Nasema sio kitu kinachofanyika kwa siku moja lakini nasema ni kitu kinachofanyika kwa nguvu ya Roho wangu. Nasema nanyi watu wangu endeleeni kuomba kwamba, Mimi Bwana Mungu wenu nitekeleze na kwamba kuregesha kwa uamsho kuje na kwamba watu wangu waamshwe na kuregeshwa, waamshwe na kuregeshwa.


Lakini nasema sio kwa uongo na utupu lakini nasema kwenye haki na utakatifu na kweli kwangu. Nasema kwa ajili ya hili muwe na shukrani, nasema kwa hili fanyeni kazi, nasema kwa hili jitoeni wenyewe. Kwa maana nasema na ninyi kwamba sio kazi iliyo rahisi. Kwa maana nasema dhambi za watu wangu zimepanda juu.


Nasema wameongeza dhambi juu ya dhambi, lakini nasema kama mta, lakini kusimama mahali palipo bomoka nasema kama mta, lakini nikachukua mzigo, nasema kama mki, lakini mkafanya maombezi, nasema nitakuwa na njia yangu na nasema nitaleta maregesho ya uamsho ambayo natamani. Nasema sio rahisi, nasema ni nguvu, nasema nitakuwa pamoja nanyi katika kutumia nguvu. Nasema nanyi kwamba hiyo ndio hamu yangu.


KUHUSIANA NA KANUNI NA NAFASI


Naam, ninawaambieni ninyi kwamba rejeeni kanuni nilizowafundisheni ninyi. Naam kumbukeni hata kanuni za mfuatano na amri na vyeo, kanuni nilizo wafundisheni ninyi ni za kuwalinda, kuwahifadhi, na ndio zitawatunza. Ndizo kanuni nilizowafundisheni ninyi ili kuwaweka katika njia. Zitawafanyeni ninyi ili msiweze kuondoka katika njia. Zitawawekeni ninyi katika nafasi zenu na ambapo mngekuwa.


 Ndio nime wafundisheni ninyi kanuni hizo kwa makusudi naam, hata mchwa hutenda kazi katika kanuni hizo, naam Mimi Bwana Mungu wenu ninafahamu kitu ninacho kifanya na nimewafundisheni ninyi kanuni ili mkaweze kufanya kazi kiulaini katika Roho, ili kwamba mkaweze kutenda kazi kulingana na jinsi ninavyopenda ninyi mtende kazi


KUHUSIANA NA KUWAFANYA WATU MAASKARI


Ninawaambieni ninyi ukubwa sio mavazi ya nje, lakini nawaambieni ukubwa ni tabia ambayo imejengwa ndani yenu kwa nguvu ya Roho yangu, kwa maana ninapenda kuwaambieni ninyi; kama Mimi Bwana Mungu wenu nikiwachukua wanaume wawili, na naesma kwamba mmoja alikuwa jenerali mkubwa na amevuliwa nguo zake nzuri na akavalishwa nguo kuukuu zilizochanika, nasema kwamba tabia yake itabakia.


Lakini nasema kama mwingine alikuwa mpumbavu mwenye kujitutumua na akavalishwa mavazi yake mazuri, nasema asingekuwa na tabia yeyote kwa vyovyote. Nasema asingekuwa na utukufu, kwa maana nasema kwamba ingekuwa tu katika mavazi yake na sio katika tabia yake.Nawaambieni ninyi kwamba Mimi Bwana Mungu wenu hujenga mtu wa ndani. Ndiyo nasema najenga tabia ya mtu, naam nawaambia hujenga ukamilifu na ubora. Ninawaambieni ninyi askari sio utu wa nje bali ni utu wa ndani.


Naam, hao ni askari wa kweli wa msalaba wangu, kwa maana nina waambieni ninyi kwamba kama kila mtu angevuliwa nguo zake na kila mtu akawa uchi mbele zangu, nasema mtu ambaye angekuwa askari, ni yule ambaye aliyevumilia vita.


Ninawaambieni ninyi, tafuteni ninyi kuwa askari wa kweli, tafutenikuwa askari wa kweli wa msalaba wangu. Kwa maana nawaambieni kwamba natamani wale ambao watakuwa askari mpaka mwisho.Sio askari wa kuvaa sare tu, sio askari wa kujionyesha kwa watu wengine tu, lakini wale watakaovumilia, naam kuvumilia vita mpaka mwisho. Nawaambieni ninyi tafuteni kuwa askari wa kweli.


KUHUSIANA NA KIKOSI CHA MSTARI WA MBELE


Ninazungumza na ninyi na ninasema kwamba nitawatumieni ninyi kama moto mtakatifu kwa sababu itakuwa moto watu ambao utaunguza. Nasema itakuwa ni utakatifu wangu ambao utakuja. Ninawaambieni ninyi kwamba nitakuwa na kikosi cha mstari wa mbele ambacho kimejitenga, ambao watatangaza kiwango changu, ambao watatangaza kuwa Mimi ni nani. Nasema watakuwa kama moto mtakatifu, ukiunguza ulimwengu huu..


Nasema msione aibu katika kitu kile ambacho nimewapeni, msione aibu mahali ambapo nimewaleteni, kwa maana nasema ninyi sio wafu, lakini nasema mko hai ndani yangu. Kwa ajili ya hii nipeni Mimi shukrani kwa maana nitawatumia ninyi kama moto mtakatifu, kwa maana nasema kwamba Mimi Bwana Mungu wenu nitatembea kwa moto wangu, nitatembea kwa nguvu zangu za utakatifu wangu.


KUHUSIANA NA NGUVU MAALUMU YA KUPIGA


Msifikiri kuwa ni kitu kigeni kwa jinsi ambavyo ninapenda kuwa ongoza ninyi. Kwa maana ninapenda kuwaambieni ninyi kwamba kuna nyakati ambazo nitasema "PIGA NA KIMBIA, PIGA NA KIMBIA." Na kitu ninacho maanisha katika hilo ni hiki, piga bomu na shambulia na halafu ondoka (kupiga bomu ni kutangaza kweli).

 

Nasema sio vituo vyote ambavyo navianzisha vitavyokuwa vya kukaa bila kuondoka au kubadilika, wala kuwa vya kudumu. Kwa maana ningependa kusema kuwa nitajimimina mwenyewe kwao na kama wakiwa waasi na kukataa hiyo nitajiondoa kwao. Kwa hiyo ninawaambieni ninyi msidhani kila mkakati ambao ninawapeni ninyi utakuwa mgeni. Lakini afadhali muwe watiifu kwangu na mtii maagizo yangu na maana Mimi Bwana Mungu wenu ni Mungu ninayetembea na wala sifungwi na desturi zauangalifu.


Kwa maana ninasema Mimi ni Bwana na ni Kiongozi Mkuu na Mimi ni Kiongozi katika vita hii.Ninawaambieni ninyi kwamba huwa ninalitoa neno langu na wakati ambapo hawalipokei ninajiondoa kwao. Ninawaambieni ninyi msigombane wala msiomboleze kwa ajili yao lakini afadhali endeleeni kutembea. Kwa maana utakapoacha mahali ambapo wamenikataa Mimi, nasema kwamba kutakuwepo mahali pengine pa kwenda.


Na mahali hapo inawezekana kwamba watanisikiliza Mimi. Kwa hiyo usikate tamaa kwa ajili ya Sodoma moja, ndiyo, usivunjike moyo juu ya Gomora moja. Lakini ninawaambieni ninyi endeleeni kutembea na Roho yangu.


Kwa maana Mimi Bwana Mungu wenu ni Mungu ninayetembea na wala sifungwi na desturi za mwanadamu,wala kukataa kwa mwanadamu. Ninazungumza nanyi siku hii ya leo na ningependa kuwaambieni kwamba muwe waaminifu kutoa unabii kama ninavyosema, kutangaza kama ninavyosema kwa maana ningependa kuwaambieni ninyi kwamba nimewaiteni kuwa sauti yangu na hicho ndicho ambacho ni lazima uwe mwaminifu kukifanya. Kwa maana ninawaambieni ninyi kwamba nimewaiteni ninyi kwa makusudi yangu na siyo kwa makusudi ya mtu mdhambi.


KUHUSIANA NA WITO WA MAPINDUZI


Ninawaambieni nnyi kwamba neno la mapinduzi litaendelea kwa maana nasema Roho yangu imesema, Nasema Roho yangu inaita kwa ajili ya mapinduzi, nasema watu watasikia wito, nasema watu wataanza kuinuka , nasema wataanza kutangaza kuwa ni saa ya mapindzi ya kitabia. Kwa maana ninawaambieni ninyi wazi wazi, kama watu hawakujinyoosha wenyewe kama nilivyo Mimi, nasema watu watalaaniwa. Nasema kilio cha mapinduzi kimesha kwenda katika ulimwengu wa kiroho. Nasema watu watasikia kilio. nasema watatwaa bendera ya tangazo.


KUHUSIANA NA WITO KWENYE JAMII


Nasema sio ukubwa wa jamii ambao unaleta nguvu, lakini nasema ni Roho ya umoja katika jamii. Nasema ni Roho ya umoja katika jamii kwa maana ninawaambieani ninyi ni faida gani ya mamilioni kama hawataunganishwa? Nasema ni afadhali kuwa na kiganja katika umoja wa jamii kuliko kuwa na wengi ambao ni wazururaji. Ninawaambieni ninyi msitizame ukubwa kama kitu muhimu, lakini nasema tazameni Roho ya umoja katika jamii ambayo ninatamani kuiweka kati yenu kama kitu muhimu, kwa maana nasema ni kifungo ambacho kitawafunga ninyi pamoja.


Furahini kuwa mmejaliwa kuwa jamii yangu ambayo nimewaunganisheni ninyi katika umoja wa kusudi kwa ajili ya ufalme wangu. Furahini kwa hiyo wapenzi na mtoe shukrani. Ninasema siku hii tena jaribuni, jaribuni, jaribuni tabia ya shukrani, iangalieni hiyo kama kazi mliyopangiwa, na mnipe Mimi shukrani na mnipe Mimi sifa na mnitukuze Mimi.Tafakarini tena mchwa kwa maana nasema hakuna hata mmoja ambae anapokea utukufu, hakuna hata mmoja ambaye anayepokea kutambuliwa, lakini nasema hata hivyo hufanya kazi. Nasema hufanya kazi si kwa ajili yao wenyewe bali kwa kila mmoja. Kwa ajili ya jamii yao hufanya kazi. Nasema hivyo ndivyo ninavyotamani kati ya watu wangu kwamba wangetenda kazi kama mchwa, sio kwamba wapokee kuinuliwa, lakini kwamba wakaweze kumwinua ndugu yao na kwamba nikaweze kutukuzwa katikati ya watu wangu.


Ninawaambieni ninyi tafakarini tena mchwa na muangalie nyendo zao kwa maana nasema kwamba naliweka katika dunia ili wanadamu wajifunze kufanya kazi si kwa kujiinua wenyewe wala kwa utukufu wao, lakini kufanya kazi kwa manufaa ya jamii ambapo nimewaanzilishia kwa manufaa ya wote kwa kaka zao na dada zao ili kwamba nikaweze kutukuzwa katikati ya watu wangu.


KUHUSIANA NA JAMII YA ROHO YA UNABII


Nazungumza na ninyi siku hii ya leo na nasema muwe wazi katika Roho yangu ya unabii kwa maana ninazungumza na ninyi na ninasema kwamba ninaachilia sauti yangu ya unabii katika dunia hii na inaenda kwa ujasiri na inaenda kwa nguvu na uweza wa moyo, kwa hiyo ninawaambieni ninyi mkae makini na wasikivu kwangu. Kwa maana ningependa kusema nanyi kwamba nimewaiteni ninyi kuwa sauti ya unabii, kushirikiana na ninawaambieni ninyi kwamba mtatabiri mmoja mmoja nanyi mtayatoa maneno yangu katika dunia hii. Kwa maana ningewaambieni ninyi kwamba nimewaiteni ninyi kwa kusudi hili kaeni wasikivu kwangu.


KUHUSIANA NA KUTOA VITABU NA MAGAZETI


Ninawaambieni ninyi endeleeni kutoa maandiko ambayo nimewapeni ninyi kwa maana katika maandiko hayo kunakaa Neno langu lillilo hai. Sio kwamba Neno langu limekaa hapo likipumua na kulala na kula katika magazeti, si hayo, lakini nasema Roho yangu iko haikatika magazeti hayo. Ninawambieni ninyi kwamba wengi wameguswa kwa hayo, nasema yanaenda katika mioyo yao, yanaenda katika fahamu zao na nia-zao nasema yanapenya katika ngome za adui zao.


Nasema ni chombo changu cha ajabu cha kuharibu hila za adui. Ninawaambieni ninyi endeleeni kutawanya magazeti hayo kwa sababu nasema magazeti hayo ni alama zangu za uzima. Nasema ninawapa wale ambao wana njaa. Nasema kuna wengi ambao hawana njaa kwa maana wameshiba vitu vya dunia hii; lakini nasema hamu yao ya kiroho ya kula haijaamshwa. Lakini nasema kwamba ninatumia magazeti hayo na vitabu hivyo kama vifaa vya kuamsha hamu hiyo. Hapo hiyo itakapoamka ndipo watakapo tamani chakula zaidi cha uzima.


WATU WANAKUFA KWA NJAA YA KIROHO


Ninazungumza nanyi siku hii naninapenda kuwaambieni kwamba kama mngekuwa katika hali ambapo watu wanakufa kwa njaa, ambapo watu wanakufa kwa ajili ya ukosefu mkubwa wa chakula, na nasema kwamba iwe wajibu wako kuwaandalia chakula, ninawaambieni ninyi kwamba ule uchungu na maumivu makali ya hali ungewasukuma mbele.


Nasema msingelala ndani na kuchukulia maisha kana kwamba hamuoni katika hali za jinsi hiyo.Lakini mngeruhusu ule ulazima uwasukume mbele. Ninawaambieni ninyi kwamba kama mngeweza kuona katika roho, ndivyo ambavyo mngeweza kufahamu kuwa inafanana hivyo hivyo katika saa hii. Kwa maana ninawaambieni ninyi kwamba watu wanakufa kwa ukondefu kwa sababu ya njaa ya kukosa chakula cha kiroho.


Kwa maana kweli ninasema kwamba kuna ukame katika sehemu hii kwa ajili ya mkate wa kweli.Na ninawaambieni ninyi kwamba Mimi Bwana Mungu wenu ninawagawieni ninyi mkate ili kwamba mkaweze kuwapa. Na wala usimtazamie mtu mkondefu sana kuwa mpole au kuwa amejaa uzima kwa maana hayuko hivyo. Kwa maana ninasema ndio sababu unatakiwa umpe chakula chake, ili kwamba akaweze kupata nguvu. Ninawaambieni ninyi hiyo basi ndio nafasi ambayo nimewaweka ninyi.Kwa maelezo zaidi kuhusu ACMTC TANZANIA, au jinsi utakavyoweza kujihusisha, wasiliana na Meja Frank & Elina Materu: S.L.P. 7579 Dar es Salaam, Tanzania. Barua pepe: materufrank@yahoo.com