Home || The Aggressive Vision || Prophetic Word Of The Lord || On Line Library || Current Articles and What's New
Free Literature || Visions from The Lord || More About ACMTC || Contact


MANENO YA WITO WA HARAKA WA MAPINDUZI YA TOBA!
"Na wengine matendo ya miujiza; na wengine UNABII…” (I Kor. 12:10)

MAPINDUZI

YA TOBA! #1

SEMWA Nov. 19, 2013

Ni Wakati Kwa ajili ya
MAPINDUZI YA TOBA!

N inaongea na nanyi siku hii, na nasema kama watu wangu mwenyewe waitwao kwa jina langu, watatubu kisawasawa, kwa kuona kosa la njia yao, na kujeuka kutoka kwenye uovu ambao wamehusika nao, nasema kwamba mimi Mungu aliye Hai ningeleta amani, ningeleta usalama, ningeleta nguvu kwao. Nasema kwamba ni mimi Mungu aliye Hai ambaye ninaweza kabisa kurejesha tena amani ya nchi kama watu wataenenda katika mimi. Hiyo ni kwamba, kama watarudia kujiweka wakfu, kujiweka kwa dhati kwangu, kama Mungu wao, kama muumbaji wao, na kunitumikia mimi tu.

Lakini nasema wakati wanadamu wanapochepuka kutoka kwangu, wakati nasema wanaitumikia miungu mingine mingi, wapenzi wengine, hapo nasema wataendelea kupagawa, kuteswa na chini ya maumivu katika hayo. Nasema kwamba mimi Mungu aliye Hai sifurahishwi kabisa wakati wale wanaodai kuwa ni watu wangu wanapotoka kwangu na kwenda kufanya ukahaba. Hiyo inamaanisha kwamba, wakati watakapo chagua miungu ya kipagani, njia za giza zaidi ya njia ambayo nimeiweka. Sasa ninasema mnaishi katika wakati ambapo kwangu wengi wamepotea, wamekwenda kwenye ukahaba, wamerudi nyuma. Nasema katika harakati za hayo yote, wananichukiza sana mimi.

Sasa nasema siku hii kwamba mimi Mungu aliye Hai sikuiti wewe kutoka kwangu na kuzurura, kuishi katika ukiwa, kuishi katika kutengwa na mimi. Lakini nasema kwamba nimekuita wewe kutemea kikamilifu, kuja katika kweli, katika rehema niitoayo. Nasema nimekuita wewe kuendelea kujiweka wakfu, kujiweka kwangu kwa dhati na kujitenga kwa ajili yangu, wakati wote ukiifuata njia yangu. Nasema ni mimi Mungu aliye Hai ambaye hutoa njia ambayo ni kweli na nuru, nguvu na tumaini, na rehema kwa wale waenendao kikamilifu katika mimi. Lakini nasema wakati watu watajitenga wenyewe na mimi, na kuwaendea miungu mingine, wapenzi wengine, hapo nasema watalipa kwa hilo.

Sasa nasema mnaishi katika nchi, mnaishi katika wakati ambapo ukahaba upo kila mahali. Hiyo ni kwamba, katika njia za makosa dhidi yangu, njia za ukiukwaji, katika njia ya kuchepuka kwenye kweli. Nasema kwamba wanadamu katika uovu wao wanatafuta kila kitu kibaya, kichafu, na kinajisi, na baadaye kudai kuwa yote ni sawa kwangu. Lakini nasema ni wajinga waishio kwenye udanganyifu wao walio utunga, nasema wako mbali na mimi. Sasa nasema siku hii kwamba mimi Mungu aliye Hai sikuiti wewe kutembea mbali na mimi, kwenda katika njia za wajinga, na kadhalika kuchukuliwa nazo. Lakini nasema kwamba nimekuita wewe kunyanyuliwa katika kile nikupacho wewe, ambacho ni kweli, nuru, rehema na amani niitoayo. Nasema wakati ambapo ni mimi Mungu aliye Hai ambaye utakuwa unatafuta kunipendeza, kunitii, na kunifuata ndipo utakapo letwa katika njia yangu. Nasema kwa uhakika umepewa kweli tele, na nuru, nguvu na tumaini, na amani niitoayo.

Nasema kwamba ni mimi Mungu aliye Hai ambaye kwa hakika nitakuwa ninawabariki watu wajitunzao wenyewe kwa ajili yangu. Hiyo ni wakati wale wanaodai kuwa wangu wakitembea kwa uhakika katika wakfu kwangu, ndipo nasema kwamba nitaleta amani katika nchi. Lakini nasema wakati wale wanaodai kuwa ni wangu, watanichepuka, wakienda katika njia za makahaba, wakijifanya wenyewe vitanda vya uasi, ndipo nasema kwamba nchi itateseka kwa ajili ya hayo yote.

Nasema kwamba ni mimi Mungu aliye Hai ambaye nitatamka ni nini kinachojiri kama ni kirzuri au kibaya. Hiyo iko hivi, kwa maana kwamba kama watu watatembea kwa ukamilifu katika mimi, ndipo watakapokuwa na baraka zangu katika maisha yao. Lakini nasema wakati wafanyapo ukahaba, wakati wanapochepuka, wakati wafanyapo makosa dhidi yangu, ndio hao watakao lipa kwa ajili ya hilo. Sio wao pekee, bali wengine watateseka vile vile kwa sababu watu wangu mwenyeye hawaku tunza upendo wao wa kwanza.

Nasema ni muhimu sana kwangu, kwamba watu wangu kuthibitishwa kuwa waaminifu na wa kweli katika mimi. Hiyo ni kwamba waweze kuja mbele katika kweli, katika nuru, katika rehema niliyo nayo, hata kuinuliwa katika njia yangu. Sasa nasema siku hii kwamba mimi Mungu aliye Hai sijakuita wewe kunikiuka nimi, kunitenda mimi uovu, kutoka kwangu na kwenda kufanya ukahaba. Bali nimekuita wewe kuwa mwaminifu, kuwa mkweli, kuwa unatafuta kunipendeza mimi katika yote ufanyayo.

Nasema wakati ambapo ni mimi ambaye unatafuta kunipendeza, kunitii, na kunifuata ndipo utakapo ongozwa na mimi. Ndipo unapopewa kweli, rehema, nguvu za jinsi nilivyo, kwa maana ni mimi Mungu aliye Hai ambaye mara zote nipo kukupatia wewe hayo.

Sasa nasema siku hii uonapo mtu yeyote anayejigamba na kujitutumua, na kujivuna, kana kwamba amefanya kubwa lolote, tafakari hili.

Je, ananiinua mimi, au anajiinua mwenyewe na njia zake? Sasa nasema kwamba mimi Mungu aliye Hai sijakuita wewe kuiinua nafsi yako, wala katika namna yake yeyote ile ya hila. Bali nasema kwamba nimekuita wewe kuniinua mimi, kwa maana ni mimi unayepaswa kunipendeza.

Sasa nasema siku ya leo unapo tazama uovu, ubaya, uchafu, upatikanao nchini, nasema ni mimi Mungu aliye Hai ambaye anaweza kuyaondoa kabisa. Hiyo ni kwamba, kama wale wanaodai kuwa wangu watatubu kwa uhakika, na kunirejea mimi ndipo nasema kwamba mimi Mungu aliye Hai, nitarejesha tena haki. Kwa maana nasema naweza kufanya kile ambacho hakiwezekani kwa wanadamu, na nasema kwamba ni mimi Mungu aliye Hai ambaye naweza kutiisha na kuondoa majeshi ya adui.

Lakini nasema wakati wale wanaodai kuwa ni wangu, watakubaliana na ajenda za adui nasema hakuna tumaini linaloweza kupatikana. Kwa ajili hiyo nasema siku ya leo endelea kutubu kwa ajili ya dhambi, endelea kulia kwa ajili ya haki ili irejeshwe, kwa maana nasema kwamba ninawasikia wale ambao wamesimama vizuri ma mimi.

Nasema kama utalia kwa uhakika kwa ajili ya watu kutubu, ni mimi Mungu aliye Hai ambaye anaweza kuwafanya hao wawe hivyo. Nasema vitu ambavyo wanadamu hawawezi kuvifanya, naweza kuvifanya! Kwa ajili hiyo nasema usiangalie mazingira, kana kwamba hayawezi kubadilishwa, lakini nasema niamini mimi. Nasema lia, lia, lia kwa ajili ya toba juu ya nchi, na mimi Mungu aliye Hai nitakusikia uliapo.

Kwa maana nasema kama kweli utatafuta kutembea kwa ukamilifu, kutafuta kufanya mambo yahusuyo maisha yangu, nguvu yangu, rehema zangu, ndipo mimi Mungu aliye Hai nitakapo kusikia wewe. Lakini nasema wakati watu watakapo fanya mioyo yao kuwa migumu, wakashupaza shingo zao na kutembea mbali na mimi, ndipo nasema maombi yao hayatafaa. Sasa nasema mnaishi katika wakati ambapo kiburi kimeshamiri katika kila mahali na wanaume na wanawake wamechukuliwa na hilo. Hiyo ni kwamba, wamechukuliwa katika maovu ya kiburi, nao wanalipenda sana hilo.

Lakini nasema kwamba mimi Mungu aliye Hai nitamsikia yeye anililiaye kwa ajili ya rehema, kwa yule anitafutaye, na kuniamini, na kunitumaini, kwamba ninaweza kabisa. Nasema iwapo ni mimi Mungu aliye Hai utajiweka mwenyewe kwangu, ni mimi Mungu aliye Hai ambaye nitakupa wewe maisha yangu. Lakini nasema kama ukichagua njia ya uovu uliozidi dhidi yangu, ndipo nasema unachagua giza katika nchi. Hiyo ni kwamba, kimsingi unajipeleka mwenyewe mbali na mimi, unajitumbukiza mwenyewe katika giza, na kizazi chako kadhalika.

Sasa nasema siku hii kwamba mimi Mungu aliye Hai ninadhamiria kwamba watu watembee katika nuru, waipende nuru, na walindwe kwenye nuru. Nasema kwamba nitaitoa nuru hiyo wakati watu watakapotubu na kunililia mimi.

Sasa nasema siku hii wakati mimi Mungu aliye Hai niletapo nuru, itaangaza giza na ubaya, uchafu, na asili yake ya kutisha. Lakini nasema watu wawapo kwenye mwanga hafifu kwa sababu ya makosa yao dhidi yangu, nasema wala hawaoni utisho wa giza la uovu. Hiyo ni kwamba, kirahisi hunung’unika wenyewe, hujikwaa njiani, na hawaoni vema kabisa. Nasema kwamba ni kwa sababu katika macho yao wana vifungo vilivyoletwa na dhambi na makosa dhidi yangu.

Lakini nasema wakati watu watakapo anza kutubu, na kubadili njia zao kabisa, ndipo nasema nuru itafunua giza na italifunika. Nasema hawatakuwa tena na urafiki na ushirika na matendo ya giza, lakini nasema watayachukia. Nasema watainuka katika hasira ya haki kulifukuza giza nchini.

Lakini nasema wakati watu waishipo katika vurugu, ukungu wa uovu, nasema hawaoni vizuri kabisa. Sasa nasema siku hii kwamba mimi Mungu aliye Hai ninaita kwa ajili ya watu kunirudia mimi, kutubu njia zao ovu, kuondoa kile ambacho ni kichafu mbele ya macho yangu. Nasema kwamba ninawaita wale wanaodai kuwa ni wangu, kuona kosa la njia zao, na kugeuka kutoka kwenye uovu wao, ambao wameuleta kwa maovu yao dhidi yangu.

Sasa nasema siku hii usishindwe wala usikate tamaa, lakini nasema uinuliwe katika mimi. Hiyo inamaanisha kwamba, unyanyuliwe katika nguvu ya uwepo wangu, furaha niitoayo, kwa wote watembeao kikamilifu katika mimi. Nasema uwe na shukrani kwamba ni mimi ambaye unaweza kuendelea kumtazama, kumwamini, kumtumaini, kumtii kwa maana mimi ndiye njia ya uzima.

Sasa nasema siku hii mimi Mungu aliye Hai simwiti mtu wangu awaye yote kuishi katika uchafu wa dhambi, kuishi chini ya uvuli wake. Wala siwaiti watu wangu kushiriki upotofu, kana kwamba ni jambo la fadhila. Lakini nasema kwamba nimewaita watu wangu kutembea katika haki, utakatifu ambao ninautaka na kuuhitaji kwa watu wangu mwenyewe. Nasena kwamba nawaita watu wangu kuimarishwa, kunyanyuliwa, kuongozwa na kuelekezwa mara zote na mimi. Kwa hiyo nasema siku hii usiharakishe kwenda katika njia ya wakosaji, usiwe na haraka kuwa na ushirika na wale ambao kweli wanaishi katika maskani ya walioangamia.

Lakini nasema badala yake uharakishe kupokea kweli yangu, na nuru yangu ili ukaweze kwa uhakika kuwa macho na hai katika mimi.

Hiyo inamaanisha kwamba, usikate tamaa kwangu kwa sababu unauona uovu, unaona giza katika nchi. Lakini nasema katika hayo yote nililie katika toba, ukitubu kwa ajili ya dhambi, maovu ya watu wangu mwenyewe ili kwa uhakika wakaweze kuona kosa la njia yao. Nasema wakati wenye haki watakapo nililia kwa uhakika, nasema kwamba nawasikia wao wanililiapo.

Lakini nasema wakati mwenye haki atakapokata tamaa katika kukosa matumaini, na kuchukia kwa jinsi mambo yalivyo, hapo watu watageukia wapi? Nasema hawawezi kufanya lolote bali kupiga mayowe kwenye upepo kwa maana mwenye haki amepoteza matumaini katika mimi. Sasa nasema kwamba wenye haki hawapaswi kukata tamaa katika mimi, lakini nasema wanatakiwa kuendelea kuniamini na kutumaini katika mimi. Nasema kama kweli wataendelea kushikilia hiyo hali yao kama wenye haki, wataendelea katika matumaini kwangu, kuniamini mimi, hawataaibishwa.

Lakini nasema wakati wale waliotakiwa kushikilia tumaini lao, imani yao, ujasiri wao kwangu, watarudi nyuma, watakapokaa katika njia nyingine yeyote, ndipo nasema mimi Mungu aliye Hai sifurahishwi kabisa nao. Kwa maana nasema hawapaswi kujiweka wenyewe kwa miungu mingine, wapenzi wengine, wala hawapaswi kujiweka wenyewe kwenye kukosa matumaini, kukata tamaa, katika mambo ya hovyo ambayo ni kikombe cha wajinga.

Lakini nasema kwamba wenye haki wanapaswa kujitunza wenyewe katika msimamo sahihi kwa kubakia katika wakfu na kujiweka kwa dhati katika kusudi langu katika mimi. Nasema kama mtu awaye yote atanitumainia, hataaibishwa kwa maana ataona kwamba nafanya mambo yasiyowezekana kwa wanadamu.

Lakini nasema wakati mtu atakapotegemea mkono wa mwanadamu, wakati atakapotumainia katika mazingira, katika hali au hata namna nchi ilivyo, nasema atakata tamaa katika kukosa matumaini. Nasema kwamba anatafuta miungu mimgine, wapenzi wengine, na nasema kwamba atajikuta kwenye ukiukwaji katika mimi. Nasema kwamba watu wangu wanapaswa kunijua, kunifahamu, na kutambua kuwa mimi ni Mungu mtenda miujiza, ambaye naweza kufanya yasiyowezekana na ni mimi wanapaswa kuniamini.

Sasa nasema siku hii kwamba mimi Mungu aliye Hai nadhamiria wewe uendelee kutumaini, uendelee kuamini, kuendelea kutegemea mimi. Nasema kwamba nadhamiria wewe kuniangalia mara zote, na kujua kuwa ninaweza. Nasema wakati iwapo kuwa ni mimi ambaye utanielekezea macho yako, abaye utakuwa unamwamini, utaona kuwa kila wakati tena, kila mara mafanya njia.

Lakini nasema kama unaangalia duniani, katika utupu, katika kupagawa, kwenye giza, nasema kwamba unaweza kukata tamaa katika kukosa matumaini kirahisi. Sasa nasema siku ya leo kama utafanya kweli kama nilivyokueleza, kuwa tubu hata kwa ajili ya dhambi za wale ambao walitakiwa kutubu kwa ajili ya dhambi zao wenyewe, nasema nitakusikia wewe uliapo. Nasema kwamba ni mimi Mungu aliye Hai ambaye atasikia vilio vya waliojiweka wakfu, waliojiweka kwa dhati kwangu. Nasema kama utaona kweli kosa la njia za watu, na kunililia mimi, ni kwamba mimi Mungu aliye Hai nitakusikiliza wewe.

Lakini nasema kama ukikata tamaa kirahisi tu katika kukosa matumaini na uchungu, nasena hayo yatakupeleka wapi wewe? Nasema kwamba yatakupeleka katika kikombe cha waovu ambapo utakunywa huko kukata tamaa, ubatili huo, giza hilo walilopo. Nasema siku hii tubu, lia katika toba, lia katika maombezi, na mimi Mungu aliye Hai nitakusikia wewe kama kweli umejiweka wakfu kwangu.

 JE, UMEKWISHA OKOKA? YESU NI HALISI!! OMBA KAMA HIVI.

Mpendwa Yesu, ninakuja kwako na dhambi zote nilizozitenda na ninakuonba wewe unisamehe. Niokoe mimi kutoka kwenye maangamizo ya milele katika moto wa Kuzimu. Ninakiri kwamba mimi ni mwenye dhambi ambaye siwezi kujiokoa mwenyewe.Usiniruhusu mimi nife katika dhambi zangu. Tafadhali takasa mwili wangu, nafsi na roho kwa damu yako ya thamani.Ninahitaji msaada wako na ninakuomba wewe uje na kuishi moyoni mwangu. Nataka nikutumikie, kutii amri zako na kufanya yale ambayo ni sawa. Nataka niishi kwa ajili yako kila siku na kuupokea uzima wa milele.Tafadhali niongoze na nielekeze kwa Roho wako katika haki. Nisaidie mimi kuishi maisha safi na matakatifu yampendezayo Mungu. Asante Yesu kwa kunisikia na kunijibu maombi yangu. Amina! Soma BIBLIA!

Tuandikie kwa ajili ya kupata bure machapisho yetu mengine yanayohusu HUKUMU YA MUNGU.

Tungependa kusikia kutoka kwako!
Kuomba maandiko au taarifa zaidi kuhusu sisi au jamii yetu tafadhali tutumie E-mail:

livingword@aggressivechristianity.net

 au tuandikie:

AGGRESSIVE CHRISTIANITY
HR 60, Box 11,
Fence Lake, NM 87315


Kwa maelezo zaidi kuhusu ACMTC TANZANIA, au jinsi utakavyoweza kujihusisha, wasiliana na Meja Frank & Elina Materu: S.L.P. 7579 Dar es Salaam, Tanzania. Barua pepe: materufrank@yahoo.com