Home || The Aggressive Vision || Prophetic Word Of The Lord || On Line Library || Current Articles and What's New
Free Literature || Visions from The Lord || More About ACMTC || Contact


MANENO YA WITO WA HARAKA WA MAPINDUZI YA TOBA!
"Na wengine matendo ya miujiza; na wengine UNABII…” (I Kor. 12:10)

MAPINDUZI

YA TOBA! #2

SEMWA Nov. 19, 2013

NI WAKATI WA....MAPINDUZI

YA TOBA!

N inaongea na ninyi siku hii na ninasema kwamba mimi Mungu aliye Hai sikuwaiteni ninyi kutawaliwa na kiburi, kutawaliwa na majigambo, kutawaliwa na kujidekeza lakini nasema kwamba nimewaiteni ninyi mtawaliwe na mimi. Ninasema ni mimi Mungu aliye Hai niliyemaanishwa kuwatawala, na na sio maroho machafu ya hivyo vitu nilivyovitaja.

Ninasema mnapoliruhusu lotote kati ya hayo, kwa maana kwamba ukweli mambo ya kimapepo, mnauruhusu uongo. Mnauruhusu ukatili ambao kweli utaziharibu nafsi zenu. Sasa nasema siku hii kwamba mimi Mungu aliye Hai nimewaita watu wangu kutembea kwa unyenyekevu mbele zangu, kila siku iwayo. Lakini mnaishi katika nyakati ambazo wengi wa wale waliodai kuwa ni watu wangu hawajinyenyekezi wenyewe kwangu. Ni hivi, wanakwenda kulingana na wawazo yao wenyewe ya kidini na wanapenda iwe hivyo. Nasema ukweli wanakuwa na ushirika na dunia kuliko kuwa na ushirika na mimi.

Ninasema wameyakataa maisha ya kuwekwa wakfu, kujitoa kwa dhati, na kujitenga kwa ajili yangu, ili kuzifuata njia za wajinga. Halafu nasema wanashangaa kwanini nchi yote iko gizani, nasema hiyo ni kwasababu wamelikaribisha liingie. Ni kwamba, wamekataa kuichukua nuru, kuutangaza uzima ambao ni mimi, na kutembea hivyo siku kwa siku. Lakini nasema badala yake wamezifuata hila za uvumbuzi wao wenewe wa kidini wakati muda wote huo wamekula ya dunia. Sasa ninasema siku hii kwamba mimi Mungu aliye Hai sijawaita kula ya dunia, kuishi katika makosa, katika uchafu na ufisadi wake. Ninasema kwamba sijawaita kuchangamana na wale ambao ni makahaba, ambao mara zote hujiweka wenyewe kwenye kila kitu kichafu na kiovu. Nasema wako wengi katika kizazi hiki wanadai ni watu wangu bado nasema kwamba maisha yao hayaonyeshi hivyo. Nasema wamejaa tamaa, kupenda ya dunia, na nasema, wanatimiza kusudi la maangamizi yao wenyewe.

Lakini nasema katika kizazi hiki kiovu, potofu, na kichafu kwamba ni mimi Mungu aliye Hai ambaye atasikia vilio vya wenye haki, kama watatubu kwa ajili ya dhambi za watu wangu. Hiyo iko hivi, kama wale ambao ni wangu watakuwa wakitubu ni mimi Mungu aliye Hai ambaye ataachia sikio liwasikie. Wale ambao ninawastahilisha kama wangu ni wale watembeao kwa ukamilifu. Nasema kundi la wazinzi waishivyo isivyopasa, na bila utaratibu, na bila kuridhika mbele zangu, nasema kwamba siwasikii waliapo.

Lakini nasema wale watakaoishi katika kuwekwa wakfu, kujitoa kwa dhati, na kujitenda kwa ajili yangu, nasema kwamba nitawasikia wao wanililiapo mimi. Sasa ninasema siku ya leo kwamba mimi Mungu aliye Hai siwaiti ninyi muishi, mfe na mpotee kama wajinga, kwa sababu mmetengana na mimi. Lakini ninasema kwamba nimewaita ninyi kuenenda kwa ukamilifu, kuja katika kweli, katika nuru, katika uweza niutoao, mkiwa mmefurahishwa kwa ajili ya njia yangu. Kwa maana ninasema wakati ambapo ni mimi ambaye mtakuwa mnanitazama, wakati ambapo ni mimi mtakuwa mnaniamini na kunitumaini, mtasogezwa mbele na mimi. Nasema mtapewa baraka, kweli, na nuru katika njia.

Kwa hiyo ninasema siku hii iweni na shukrani kwamba mimi Mungu aliye Hai atawapeni fursa ya kulia katika toba, kulia kwa ajili ya kurejeshwa kwa haki, kwa ajili ya nuru yangu kurejeshwa. Ninasema kama wale ambao ni mali yangu kwa kweli watakuwa wanatubu kwa unyenyekevu, nasena kwamba wengine wataletwa katika hilo. Kwa maana nasema ni saa ya mapinduzi ya toba, ambayo ni kutubu kwa ajili ya uovu, kwa ajili ya dhambi, kwa ajili ya uchafu, kwa ajili ya giza, kwa ajili ya uovu ambao upo kila mahali. Naasema watu watakapojipanga wenyewe kutubu na kutubu, na kutubu, hata kama sio kwa dhambi zao wenyewe, nasema kwamba ninasikia.

Ninasema siku ya leo kwamba mimi Mungu aliye Hai hutafuta masalia ya wenye haki ambao kweli watakuwa katika toba, katika toba, katika toba kwangu. Ninasema wakati mwanamume au mwanamke yeyote atajiweka mwenyewe katika mahali pa maombezi kwa ajili ya waovu, kwa ajili ya uovu, kwa ajili ya uchafu na kulia katika toba kwa ajili ya hayo, ndipo nasema kwamba mimi Mungu aliye Hai nitakapowasikia waliapo. Wakati kweli nisikiapo kilio cha wenye haki, ndipo nasema kwamba nitawafunika hata wale ambao ni waovu, kwa ushawishi wa hamu ya kutubu.

Nasema ni mimi Mungu aliye Hai ambaye anaweza kabisa kufanya kazi kubwa na ya kushangaza. Lakini nasema wakati wale walio simama vizuri na mimi watakapo ruhusu unajisi, au kuruhusu kukata tamaa, hayo ni katika nchi, wanafanya nini? Nasema wanaizimisha nuru, wanauzimisha moto, wanaizimisha shauku yao kwangu.

Nasema kwamba wao wenyewe kwa hilo wanakuwa wasio haki kwa sababu wameshindwa kuilinda imani yao kwangu. Hiyo ni kwamba wametazama katika mazingira, wakajipatia wenyewe kukata tamaa, na kwenye dhambi ya kutokuamini.

Sasa ninasema siku hii kwamba mimi Mungu aliye Hai siwaiteni ninyi kukata tamaa, lakini nimewaita kuendelea kuamini, kuwa na tumaini kwangu. Nasema kwamba nimewaita ninyi kuwa na shukrani kwamba ni mimi ambaye mtaweza kumtazama, na kumwamini, na kumtegemea. Kwa maana nasema kama mtaendelea kuangalia kile ambacho mimi Mungu aliye Hai niwapacho, nasema kwamba, nawapeni uzima kamili. Nasema kwamba nawapa rehema, na kweli, na nuru katika njia siku kwa siku.

Kwa hiyo nasema siku hii tambua kuwa mimi Mungu aliye Hai nawaita ninyi kubakia katika mahali pa wakfu, kujiweka kwangu kwa dhati na kujitenga kwa ajili yangu. Hiyo imanaanisha, sio kujiweka wenyewe kwa dunia, hata kwa kile kionekanacho hakina hatia, wakati humaanishwi kufanya hivyo. Lakini nasema unamaanishwa kujiweka mwenyewe katika nira ya utii kwangu, lakini unaweza kweli kuwa katika nafasi ya maombezi, dhidi ya uovu ambao unameza nafsi za watu katika nchi hii. Nasema kama utafuata nia ya Roho wangu haswa na kwa kweli, na kulia katika toba nasema kwamba nitakusikia wewe uliapo. Lakini nasema kama ukitikisa kichwa chako na kusema kwamba haiwezekani kuwa, ndivyo utakavyojiweka katika kutokuamini.

Sasa nasema siku hii kwamba mimi Mungu aliye Hai hupendezwa wakati watu watakapoamini katika mimi, zaidi ya kupita mazingira. Hii ina maana kwamba, wakati watakapoona kweli kwamba sio kwa jinsi wajisikiavyo au jinsi wadhanivyo masuala huwa ndicho kinachojalisha bali utii wao kwangu. Hiyo ina maana kwamba, inajalisha kwangu kwamba watu wangu watanitii mimi na kufanya kama niagizavyo, na kutembea kikamilifu katika mimi. Ninasema kwamba haijalishi kwangu kwa maana kwamba nasikizisha sikio pia wakati watu wangu wananung’unika na kulalamika, katika kujidekeza na kiburi, katika kukosa utii mbele zangu.

Sasa nasema siku hii kwamba mimi Mungu aliye Hai huwaita watu wangu kuwa tayari kutubu saa yeyote ile, nitangazapo hitaji hilo kwao. Kama wale ambao ni wangu hawatakuwa wamejazwa na haki yao wenyewe na kiburi lakini wakajinyenyekeza mbele zangu, hapo nasema kwamba haitakuwa ngumu kwao kutii amri zangu. Lakini nasema wakati mwanamume au mwanamke awaye yote amejaa mambo yake mwenyewe, amejaa majivuno, kiburi, ukatili ambao atauonyesha dhahiri, nasema ndipo hapo ni aibu katika jina langu. Nasema hatapokea amri zangu kwa furaha, lakini nasema atazichukia. Sasa nasema siku hii jipimeni wenyewe kama mna kinyongo kwa ajili ya mimi kuwarudi, maelekezo yangu, amri zangu kwenu, kwanini iko hivyo?

Nasema hiyo ni kwa sababu mnaruhusu mnyama kuvimba katika kiburi, kuvimba katika kujidekeza, na ubatili, na kuwafanya ninyi kujiona ni bora zaidi ya jinsi mlivyo. Lakini nasema kama mtapokea amri zangu kwa unyenyekevu mtaona kwamba kweli zenyewe zitawaleteeni uzima. Nasema ndivo katika wakati huu mwovu, kwamba mimi Mungu aliye Hai ninawataka ninyi kufanya maombezi na kutubu kwa ajili ya dhambi za waovu. Na, kutubu kwa ajili ya dhambi za wale ambao hudai ni watu wangu, bado nasema kwamba wanaishi kwa ajili ya dunia. Nasema vile vile kutubu kwa ajili ya wale wadaio kuwa ni watu wangu bado wanaabudu mungu wa nafsi.

Kwa maana nasema kuna uovu uliozidi na mabaya ambayo yanahitaji kutubiwa, kabla mimi Mungu aliye Hai sijarejesha nuru katika nchi. Nasema kama watu wangu wa kweli watafanya maombezi ki ukweli na kutubu, na kutubu, na kutubu, nasema kwamba ni mimi Mungu aliye Hai ambaye kweli nitatembea kwa mamlaka yangu, nitatembea kwa nguvu yangu ya muujiza

Nasema kwamba vitu ambavyo vinawezekana kwa mwanadamu, ndiyo wanaweza kufanya vitu hivyo. Lakini nasema kwamba vitu ambavyo haviwezekani kwa wanadamu vinaweza kufanyika tu kupitia mimi. Kwa hiyo nasema uwe mwaminifu kwamba udumu kuamini na kutumainia katika mimi, kwa maana mimi ndiye niwezaye. Nasema uwe unaniangalia mimi, kama mweza, mshindi, Mungu mmoja wa kweli.

Nasema wakati ni mimi ambaye utaendelea kunitazama kwa imani, katika tumaini, kwa ujasiri, ni mimi Mungu aliye Hai ambaye atatembea kwa mkono wangu wenye nguvu. Ni mimi Mungu aliye Hai atakayefunua tena na tena, na tena nguvu zangu za utendaji za muujiza ambao hupita ajenda ya uovu.

Kwa hiyo nasema siku hii acha tumaini lako, ujasiri wako uwe kwangu, endelea kuniamini mimi. Hiyo ni kwamba, usirudi nyuma, usiporomokee kwenye kujidekeza, kwa sababu ya uovu wa wakati.

Nasema usiwe na kiburi kiasi cha kushindwa kupiga magoti, kulia katika toba ya dhambi ambazo hata huhukumiwi nazo. Nasema kwamba katika saa hii ninatafuta wale watakao simama katika mahali palipobomoka na kulia, na kulia, na kulia katika toba kwangu.

Nasema kwamba wale watakaosimama mahali palipobomoka watahesabiwa kama wenye haki mbele zangu kwa sababu wameona uovu, kwa sababu wamesikia uchafu, kwa sababu hata wametazama uovu, bado nasema hawajaushiriki. Lakini nasema watasimama mahali palipobomaka, ili kunifanya mimi Mungu aliye Hai nisiangamize kabisa nchi.

Sasa nasema siku hii kwamba ni mimi Mungu aliye Hai ambaye ninaweza kabisa kutembea kwa nguvu yangu iliyo hodari, na watu wala hawajui kilichoyaleta. Lakini nasema kwamba mimi ni Mungu mtenda miujiza, ambaye huinua mataifa juu, na huyashusha chini. Nasema kama taifa lolote litakuwa katika hali ya toba ni mimi Mungu aliye Hai ambaye ninaweza kutoa rehema.

Lakini nasema kwamba toba ni lazima ianzie kwa wenye haki, ambao ni wale waliopo katika nyumba yangu. Hao ni, wale wadumuo katika mimi, wanaonishiriki mimi, na kuishi ndani yangu. Sasa nasema siku ya leo usione aibu kukiri dhambi, makosa ambayo unayaona kila mahali. Nasema usione aibu kusikitika kwa yale mambo hata kama hujayafanya. Nasema kweli utakapojiruhusu mwenyewe kutumiwa katika huduma ya maombezi, moyo wako utaumia kama ninavyoumia mimi. Kwa maana nasema utaona ubaya, unyonge, uovu ambao watu wameuchagua zaidi yangu. Nasema utaona ni kiasi gani walivyonijeruhi, ni kwa jinsi gani walivyojaribu kuniharibu, wakati nilikuja tu kuwaletea wao uzima. Sasa nasema siku hii usijitutumue katika moyo wa kutokuamini, wala kujitutumua katika uchungu wa chuki lakini nasema badala yake mjiruhusu wenyewe kutumiwa na mimi. Nasema siku hii msione aibu kukumbuka kuwa ni mimi Mungu aliye Hai na mimi peke yake ambaye naweza kubadilisha jinsi mambo yalivyo.

Nasema wanadamu vile vile kwa juhudi zao zote ni bure kabisa, kwa maana nasema kwamba uovu unalingana katika nyakati hizi. Lakini nasema wakati wale ambao ni mali yangu watapiga magoti, watatubu kweli, ndipo nasema kwamba ni mimi Mungu aliye Hai ambaye nitasikizisha sikio langu katika hilo. Sasa ninasema siku hii kwamba mimi Mungu aliye Hai sikuiti wewe kuwa mshirika wa unyonge, uovu, ufisadi uliopo kila mahali.

Wala sikuiti wewe kukata tamaa na uendawazimu usiofanya lolote la maana katika ujinga wa kukosa matumaini na kudhani hakuna kitu cha kufanya. Nasema maadam mwanadamu ana pumzi kuna mambo mengi ambayo aweza akawa anayafanya kuonesha toba yake mbele zangu. Ni kwamba, sio tu toba kwa ajili ya dhambi zake, lakini kwa ajili ya dhambi za wengine vile vile.

Sasa nasema siku ya leo wakati unapotafakari kipindi nilipokuja kama mwanadamu, nilikuja kama mwombezi, nilikuja kama neema, nilikuja kama malipo ya dhambi zao. Nasema nilibakia katika mahali ambapo Baba yangu alikuwa amenikusudia na nilimaliza mwendo wangu.

Nasema kwamba Baba alisikia jinsi ilivyokuwa ambayo niliyasema, nilichokifanya, na hata nilivyoishi na kufa. Nasema ilikuwa ni kwa sababu niliyatoa maisha yangu kikamilifu katika mapenzi ya Baba yangu na nilisimama katika mahali pa wenye dhambi wakati sikutenda dhambi kabisa. Sasa nasema siku ya leo usiwe sana na haki yako mwenyewe kiasi cha kukataa kutubu kwa ajili ya dhambi za wengine wapoteao katika hizo. Nasema wako wengi ambao wamejaa haki yao wenyewe katika saa hii ya uovu, na hawataki kuangalia.

Lakini nasema kwamba ukweli wa hilo ni kwamba hutakiwi kudharau mahali pa unyenyekevu ambapo nitakuweka kama unavyofanya maombezi kwa ajili ya rehema zangu kuja. Nasema kuwa mimi Mungu aliye Hai ninapendezwa wakati wenye haki watakapopiga magoti, wakati watakapotubu, wakati watakaponililia mimi. Nasema siku hii uwe na shukrani kuwa sehemu ya mapinduzi ya toba ambayo mimi Mungu aliye Hai nimeyaleta.

 JE, UMEKWISHA OKOKA? YESU NI HALISI!! OMBA KAMA HIVI.

Mpendwa Yesu, ninakuja kwako na dhambi zote nilizozitenda na ninakuonba wewe unisamehe. Niokoe mimi kutoka kwenye maangamizo ya milele katika moto wa Kuzimu. Ninakiri kwamba mimi ni mwenye dhambi ambaye siwezi kujiokoa mwenyewe.Usiniruhusu mimi nife katika dhambi zangu. Tafadhali takasa mwili wangu, nafsi na roho kwa damu yako ya thamani.Ninahitaji msaada wako na ninakuomba wewe uje na kuishi moyoni mwangu. Nataka nikutumikie, kutii amri zako na kufanya yale ambayo ni sawa. Nataka niishi kwa ajili yako kila siku na kuupokea uzima wa milele.Tafadhali niongoze na nielekeze kwa Roho wako katika haki. Nisaidie mimi kuishi maisha safi na matakatifu yampendezayo Mungu. Asante Yesu kwa kunisikia na kunijibu maombi yangu. Amina! Soma BIBLIA!

Tuandikie kwa ajili ya kupata bure machapisho yetu mengine yanayohusu HUKUMU YA MUNGU.

Tungependa kusikia kutoka kwako!
Kuomba maandiko au taarifa zaidi kuhusu sisi au jamii yetu tafadhali tutumie E-mail:

livingword@aggressivechristianity.net

 au tuandikie:

AGGRESSIVE CHRISTIANITY
HR 60, Box 11,
Fence Lake, NM 87315


Kwa maelezo zaidi kuhusu ACMTC TANZANIA, au jinsi utakavyoweza kujihusisha, wasiliana na Meja Frank & Elina Materu: S.L.P. 7579 Dar es Salaam, Tanzania. Barua pepe: materufrank@yahoo.com