Home || The Aggressive Vision || Prophetic Word Of The Lord || On Line Library || Current Articles and What's New
Free Literature || Visions from The Lord || More About ACMTC || Contact


Mapinduzi ya Toba!

Sehemu ya 1

Gen. James Green

TUNAKWENDA kuwa katika Yeremia 26 leo, na tutarukia nyuma kwenye sura ya 7, halafu nataka kuanza mafundisho ya "MAPINDUZI YA TOBA" leo. Roho amekuwa akiyatoa Maneno ya unabii, mara-mbili-kwa siku, kwa kama juma moja. Na si tu kama unapenda…bali una HITAJI kwenya kwenye tovuti hizi: www.youtube.com/user/shimrana,www.youtube.com/user/operationdevastation, na www.youtube.com/user/righteous1revolution.

Utakuta Operesheni Teketeza na Mapinduzi ya Toba hapo juu yakiwa na mengi ya Maneno ya unabii ambayo Mungu alitupa sisi. Na utaona mengi ya vielelezo hasa Operesheni Teketeza. Tumekuwa tukifanya hivi kwa muda wa mwaka sasa, kila siku---kila siku iwayo tumekuwa tukiweka vitu juu hapo kukuonyesha wewe, usiyeamini, kile Mungu awezacho kukifanya katika taifa… na dunia.

Kuna rekodi nyingi za majanga ---- kila aina ya MAJANGA ambayo ungeweza kuyafikiria yaliyoonyeshwa hapo ---- NA HAYO NI KUTOKA KWA MUNGU. Mungu anafanya hivyo ---- Analileta hili. Sio shetani, ni Mungu anayefanya haya. Na, kwa kweli shetani anapenda sana wakati Mungu anapowaangamiza watu na wote wakaenda Motoni…kwa sababu atakwenda kuwa mpweke huko chini bila wao.

Lakini kwa vyovyote vile, kwamba Operesheni Teketeza imekuwa ikiendelea mbele, na itaenda kuendelea. Lakini SASA MAPINDUZI HAYA YA TOBA YANAONGOZA, na tunapokea Maneno sasa ambayo unaweza kuyapata kwenye mitandao ya habari, na vile vile katika machapisho ya Maneno ya Roho ambayo tunachapisha. Kadhalika, katika mengi ya mafundisho yetu, utayakuta Maneno haya.

Hivyo, ningetaka kila mtu kwenda hapo na kuyasikiliza maneno hayo, ayatafakari Maneno hayo, na kuyatii Maneno hayo---- kwa sababu Mungu hafanyi mzaha. Kanisa limeangamizwa sana LIMEANGAMIZWA kiasi kwamba wala halitambui hata kama Mungu amekasirika; sasa huo ndiyo ukweli.

Usikilize baadhi ya haya Maneno ambayo Mungu anatuambia sisi. Kama utasikiliza kwa makini, kama mojawapo tulilolisikia leo, watu hawatambui kwamba Mungu amekasirika, hawatambui kuwa wanahitaji toba, na hawatambui kuwa wamemkasirisha Mungu. Na Israeli, kama tutakavyokwenda kujifunza walikuwa katika hali hiyo hiyo mara nyingi.

Wamefika mbali sana na Mungu kutoka kwenye ibada zao za sanamu, uzinzi wao, anasa zao, kufurahia kwao dunia, na kufanya kwao kila kitu wapagani walichokuwa wakikifanya, na mengi zaidi, kwamba wala hawakuelewa ni kwanini Yeremia, Ezekieli Isaya, Amos na Hosea na manabii wote, mara zote WALISHAMBULIA dhambi zao. Wanasema, “Sawa, kwamba tunachokifanya, unatakiwa kukisema hivyo mara kwa mara dhidi yetu na jiji letu?

Sawa, Marekani iko katika hali hiyo sasa, rafiki. Na Mungu hatanii. Kama watu wa Mungu----wafanyao maombezi wa kweli, watu wa kweli--- hawataomba kama anavyoagiza sasa hivi, Mungu atakwenda kuiangamiza nchi hii sasa hivi, Mungu anaenda kuiharibu nchi hii haraka kuliko unavyoweza kufumba jicho lako.

Sasa, ana vipindi katikati ya majanga haya makuu, na ametuambia “Ninakwenda kuleta majanga” na mtayaona: upepo wa sunami, mafuriko, moto, ukame, njaa, mambo ya kutisha, na UHARIBIFU WA KUTISHA wa mali na nchi yenyewe.

Upotevu wa maisha ya watu umepungua (kidogo sana), lakini huo utaongezeka baadaye kama watu hawatatubu. Na baadaye atasitisha, na itaelekea kana kwamba hakuna kitu kinachoendelea…kwa muda. Mungu anatuambia kwamba anaangalia kama watu wanasikia ishara hizo za maonyo kwamba amekasirika. Na HAPANA, tuna Laana ya Msamaria, ijulikanayo kama Mkoba wa Msamaria wakitembea na malori yao makubwa, wakitoa kwa watu visarafu kidogo na vipaketi kidogo, na kuwakumbatia na kuwabusu, wakiwaambia ni kwa jinsi gani “Mungu anavyowapenda, na ni shetani anayafanya hayo

Shririka la Billy Graham na matapishi yaliyopo hapo si lolote bali ni mapepo katika miili ya binadamu, yakifanya kazi moja kwa moja dhidi ya Mungu.

 Rick Warren, Joel Osteen, wote hao wanahusika kwa kutengeneza pesa nyingi kwenye majanga ya Mungu. Wakati Mungu aletapo majanga haya---- OPERESHENI TEKETEZA; ANAFANYA HILO KUWAAMSHA WATU---ILI kwamba wakaweze kutubu dhambi zao, ili wakose Jehenamu, na kwenda Mbinguni. Hilo ni kusudio la Mungu.

 Sio kusudi lake kwa watumishi wake kupitapita na kuwaambia watu kwamba Mungu anawapenda, na kuwafanya wajisikie vizuri katika dhambi zao. Hicho ndicho watu hawa wamekuwa wakikifanya kwa muda mrefu. Kila wakati kunapokuwa na majanga, wanakimbilia hapo, wanakimbilia pale, wanakumbatia watu, wanawaambia ni kwa kiasi gani Mungu anawapenda na mambo yote haya. NA HAWATAWAAMBIA WATUBU; HAWATAWAAMBIA HASIRA YA MUNGU. Sawa, hilo sio la kawaida, na hawatapata michango yeyote. Wanafanya haya kupata michango…kila majanga.

Kama ambavyo tumekuwa tukihubiri kuanzia mwanzoni wa miaka ya 80, MAJANGA NI BIASHARA KUBWA KWA WAHUBIRI. Wanatengeneza fedha nyingi sana. Na watainuka katika maonyesho ya TV zao na kulia (vizuri kiasi cha kuwadanganya) kuhusu ni kwa kiasi gani wanavyojali nafsi zote zinazoteseka, na “Tunataka kuwasaidia watu hawa”.

Na wakakuwa na maonyesho maalumu ya TV kwa ajili ya kuwaomba watu wawape. Ndipo, kana tuseme dala milioni 5, hadi milioni 10 mpaka hata dola milioni 50-60 zinazokusanywa, watachukua kiasi kidogo, na kununua vifurushi vidogo vya China ambavyo ni rahisi. Wanachukua zinazobaki, na kuziweka kwenye akaunti zao nene za benki----ili kwamba wakaweze kuishi maisha yao ya anasa, na wakaweze kujenga sanamu kwa mwanzilishi wao ----kama Billy Graham, na kuwa na nyumba ya makumbusho kama “Billy Graham na mambo yote makubwa aliyofanya.” Na hata ile sura za zamani bado haijafa. Na wakamjengea nyumba ya makumbusho, wana sanamu waliyomjengea, na wana barabara iliyopewa jina lake; na inaendelea. Ibada ya sanamu na uzinzi ni mkubwa.

Sasa, ninautoa ujumbe huu Novemba 24th, 2013; kuna baridi huko nje…ndiyo maana nimevaa jaketi zuri la joto. Umekuwa ukivuma upepo mkubwa masaa 48 bila kusimama, na tuna barafu imeanguka chini; tuna hali ya hewa ya baridi. .

Na Mungu anatuambia “Hii ni hali tu ya nchi.” Hakua anaongea kuhusu hali ya hewa. Alikuwa akionyesha ukweli kwamba HALI YA KROHO NI NYUZI 0 ---BARIDI KWA MUNGU-----ikiganda kumweleke Mungu; sio ya joto kumwelekea Yeye. Tunaishi katika taifa ambalo limemwacha Mungu, na hali ya hewa ni baridi.

Hivyo, mambo yataenda kuwaka moto wakati moto wa Mungu wa Mapinduzi utakapowashwa---kama watu wasipotubu. Unasema, “Sawa, umekuwa ukiwatisha watu kwa muda mrefu” Tumekuwa tukiwatisha watu kwa sababu Mungu ametuambia hilo; na wewe unaona Mungu anachokifanya. Kama huamini, angalia tovuti hizo hapo juu, angalia kwa jicho lote, MWANGALIE KILA MMOJA kwenye Operesheni Teketeza iliyowekwa hapo. Ziko jozi mamia hapo.

Angalia vizuri majanga yote. Angalia vizuri jinsi anavyosawazisha uataarabu wote, miji yote, majiji yote…kila jengo linabomolewa. Hii ilitokea wiki iliyopita katika Illinois---mji wote ulisawazishwa, kila nyumba mahali pale ilibomolewa, huo ni mkono wa Mungu. Sasa Mungu hageuzi hali yake ya hewa kwa watu waovu, wala kwa shetani. Na hata akiwatumia watu waovu, au shetani, Mungu bado anatawala.

Sawa, kwa lililosemwa na kutendeka, na tuendelee na ujumbe huu leo…katika hali hii ya hewa baridi, vilevile angalia kama Mungu anachosema kama ni kweli.

Sasa, tunazungumzia kuhusu toba. Haya ni majira sio ya kufanya shamra shamra, sio kumsubiri santa claus akitokea mwezi ujao---na beji lake la madoli na kuwapa walionavyo, na matajiri, wakati watoto maskini hawapewi chochote. LAKINI, HAYA NI MAJIRA AMBAYO MUNGU ANALETA, KIPINDI CHA MUDA AMBAO WATU WAKE WALITAKIWA WAWE KWENYE MAOMBI KATIKA MAOMBEZI KILA SIKU KWA AJILI YA DHAMBI —sio kwamba tunazitenda, lakini dhambi ambazo wengine wanazitenda, na kadhalika tunatubu kwa ajili ya dhambi zetu wenyewe.

Na kama ukisema, “Sawa, sitaki kuwaombea kwa sababu ninaamini wanastahili kile wanachokipata”. Hivyo sivyo Mungu anavyosema. Kuna wakati nilistahili kile nilichotakiwa nikipate, nacho ni Motoni, na Mungu alinirehemu. Alikuwa na rehema kwako, hivyo inabidi kukumbuka rehema. Na Mungu anafahamu ni lini rehema zake zitakwisha. Mpaka zitakapokwisha tunaomba rehema, wakati mlango utakapofungwa, mpendwa, umefungwa—hakuna mtu atakayekwenda kuufungua mlango. Wakati safina ilipofungwa katika siku za Nuhu, ilikuwa imefungwa. Mungu aliufunga mlango. Aliwafungia kwenye safina.

Mungu aliufunga mlango, nao ulifungwa. Maji yalipoanza kujaa, na watu wale wakichukuliwa----sio katika hadithi nzuri ya unyakuo, lakini walichukuliwa na mafuriko---Nina uhakika walikuwepo watu mamilioni waliotamani kama wangelimsikiliza Nuhu, yule mjinga wa zamani aliyekuwa anahubiri pale. Hakukuwahi kuwepo maji duniani kama katika kipindi kile; walidhani ilikuwa amechanganyikiwa: “Hebu mtazame yule mzee kichaa na familia yake hapo akijenga mtumbwi wake mkubwa…kwa ajili gani? Tuko nchi kavu”

Sawa, najua nini ILIKUJA. Inasemekana: “katika siku moja pekee (ambayo Mungu aliiteua) kwamba mlango ulifungwa” Hivyo, tuko mahali katika muda ambapo mlango wa safina uko wazi kwa yeyote atakayetubu, lakini wakati huo huo, Mungu bado analeta Operesheni Tokomeza yake, na bado anaharibu. Bado anaua watu sasa hivi. Bado anaiharibu nchi, na mambo yake, na vitu---akijaribu kuwafanya watu watubu. Lakini ni wajibu wetu angalau kuwaombea wale watajao kuwa ni Wakristo lakini wapo mbali na Mungu. Ni kweli, tunawaombea wasioamini ambao hawamfahamu Mungu.---ili kwamba wamfahamu Mungu---ili kwamba wamjue Yeye. Sasa, katika Yeremia 26, tunasoma hapa juu ya habari ya wafalme watatu wa mwisho kabla ya Wababeli mwisho kuiangamiza Yerusalemu. Mungu alikuwa akiionya Israel kwamba kama hawataacha kutenda dhambi, Mungu angekwenda kuwaangamiza; na akamwinua Nebkadneza kuingia.

Hatua ya kwanza wakaanza kuvizia. Wakaingia na kuteka nyara baadhi ya miji, wakawachukua watu wengi katika minyororo, na kuwapeleka Babeli. Ezekieli, Danieli, na wengineo walikuwepo katika lile wimbi la kwanza la utumwa wakati Mungu aliporuhusu Wababeli kuingia. LAKINI, BADO HAWAKUTUBU, Wakampata mfalme mwingine wa kutawala kwa muda mfupi. Hawakumtii Mungu, na ndipo jeshi la Nebkadneza likaja tena na kufanya uharibifu mkubwa: wakalichoma hekalu, wakazichukua hazina zote kwenye hekalu, wakavisafirisha, wakawachukua wafungwa wengi, na waliteketeza. Na mfalme wa mwisho, Zedekia, alikataa kumsikiliza Yeremia. Alikataa kumwamini Yeremia au kusikiliza kile Yeremia alichokuwa akisema.

Ninafikia mwisho wa kitabu cha Yeremia, lakini habari yote inasema kwamba WALA HAWAKUTUBU, HAWAKUSIKILIZA, WALIANGAMIZWA NA MUNGU; na Mungu alitumia nguvu ya adui kufanya hiyo kazi. Mungu yeye binafsi hakuja kuifanya. Mungu alitumia mashambulizi ya adui kufanya hivyo. Nawe unadhani Marekani inazidi hapo?

 Ingekuwa afadhali kama ungeliamka. Kama Mungu anataka kutumia tauni na magonjwa, atayatumia. Kama akitaka kutumia vimondo kutoka angani, na kuipiga miji, kuwasha moto, na kuporomosha vitu, atafanya hivyo.

 Kama akitaka kuuleta ukame wote ukaushe kila kitu, au chakula chote, kusiwemo na chakula, au moto wote kuunguza kila kitu, atafanya hivyo. Au, kama akitaka watu waovu kwa namna ya jeshi, au kuinus jeshi KATIYAO…na rais akiongoza, atafanya hivyo sana.

Sawa, hebu tuangalie saa hii kwa muda katika mstari wa 2: “Bwana asema hivi, Simama katika uwanja wa nyumba ya Bwana, useme na miji yote ya Yuda, wajao ili kuabudu katika nyumba ya Bwana; sema nao maneno yote ninayokuamuru kuwaambia,…”

Oh, nataka kuwa nabii. Nataka kuwaeleza watu hao ni nini cha kufanya; nataka kutoa unabii” Oh, ninauhakika unataka kutoa unabii, na kueleza ya baadaye. Labda wewe kadhalika unaweza kusaini vitabu pale Barnes na Nobles,

ya watazamaji. Na wewe upo juu hapo, nabii wa Mungu ukitoa ujumbe---wakati ukikusanya mamilioni ya dola, na kuishi katika maraha; na mwili wako ukinuka dhambi zako mwenyewe ambazo hazijatubiwa----nina uhakika Mungu hataenda kukutumia wewe!

Inashangaza ni watu wangapi wangependa kutoa unabii na kupenda kuwa nabii. Unafahamu kazi ya kweli ya nabii ilivyokuwa? Haikuwa kueleza yatakayokuja, hiyo ni sehemu ndogo, KAZI YA NABII ILIKUWA KUWAKUMBUSHA WATU DHAMBI ZAO---KUWAKUMBUSHA WATU AHADI ZAO NA AMRI ZA MUNGU KWAO; HAYO NDIYO WALIYOTAKIWA KUYAFANYA.

Mungu aliwaamuru kufanya hivyo. Waliamriwa kwa sababu walikuwa chini ya amri. Huwezi kuwa nabii wa kweli wa Mungu kama unaishi katika dhambi, na unaenda kila mahali kutenda kila dhambi---wakati ukinyooshea kidole cha mwili wako unaonuka dhambi kwa wengine kwa kuzifanya. Tunao wa kutosha wa jinsi hiyo hapa kwenye nchi ya ba-ba.

Sawa, walisema “Usizuilie---neno lolote. Usifupishe na usijadiliane. Usiseme, “Sawa, samahani, lakini kweli nisengependa kusema hili, au samahani, natakiwa niongee suala hili na wewe kuhusu uzinzi wako na ibada yako ya sanamu, na uuwaji wako wa watoto na umwagaji wako wa damu, na dhambi zako za ngono, na yote haya. Samahani, nimetakiwa kukueleza haya, lakini ni Mungu ameniamuru, na hapa inaendelea…” Yeremia akayaeleza Maneno yote.

Naye akawaambia mstari wa 4. “Naye akawaambia, Bwana asema hivi, kama hamtaki kunisikia, kwenda katika sheria yangu, nilivyoiweka mbele yenu kuyasikizisha maneno ya watumishi wangu, manabii, ninaowatuma kwenu, naam, nikiondoka mapema na kuwatuma; lakini ninyi hamkuwasikiliza;…” Tazama, Mungu amekuwa akirudia rudia suala hili kwa muda mrefu----Najua katika kazi hii amefanya hivyo.

Sasa, sifahamu kuhusu watu wengine hapo kwa maana ni vigumu kumpata mtu yeyote aliye sambamba na Mungu. Lakini, nafahamu wako watumishi ambao Mungu anawatumia kusema, lakini ni kidogo sana, na hakuna anayesikiliza.

Sasa, mstari wa 6 ni somo langu jingine leo: “Basi nitafanya nyumba hii kuwa Shilo, na mji huu nitaufanya kuwa laana kwa taifa zote za dunia.” Sasa, ni nini kilitokea Shilo kiasi cha Mungu kuitumia kama kielelezo katika hilo,

 

“Naye akawaambia, Bwana asema hivi, kama hamtaki kunisikia, kwenda katika sheria yangu, nilivyoiweka mbele yenu kuyasikizisha maneno ya watumishi wangu, manabii, ninaowatuma kwenu, naam, nikiondoka mapema na kuwatuma; lakini ninyi hamkuwasikiliza; Basi nitafanya nyumba hii kuwa Shilo”

Sawa, kama ukiweka kidole chako hapo rudi nyuma sura ta 7, tutaona kitu hapa. Sasa, kumbuka kwamba hii ni sehemu ya 1 katika mafundisho ya “MAPINDUZI YA TOBA.” Kama ukianza kusoma katika mstari wa 1 sura ya 7, na ukaelewa hilo, anazigonga dhambi zao: maneno ya uwongo, kuiba, kuua, uzinzi, kuapa kwa uwongo, kumfukizia Baali uvumba, na kuifuata miungu mingine. Ndicho kinachomchukiza Mungu---anachukia kile walichokuwa wakikifanya.

Na baadaye katika mstari wa 10 anaongelea kuhusu machukizo. Na tena mstari wa 12 unasema, “Lakini enendeni sasa hata mahali pangu palipokuwapo katika Shilo, nilipolikalisha jina langu hapo kwanza, mkaone nilivyowatenda kwa sababu ya uovu wa watu wangu Israeli.”

Sawa, hapa ni Yeremia wakati mwingine, katika siku nyingine, labda katika mwezi hapa, njia kabla katika mstari wa 26 ambapo anaongelea kuhusu Shilo. Kwa kweli, kumbuka, manabii walikuwa wanatoa ujumbe kila siku kwa mfalme na kwa watu. Haikuwa mara moja kwa mwaka kwenye krismas, au siku ya shukrani, na pasaka hapo…lakini KILA SIKU.

“Naye akawaambia, Bwana asema hivi, kama hamtaki kunisikia, kwenda katika sheria yangu, nilivyoiweka mbele yenu kuyasikizisha maneno ya watumishi wangu, manabii, ninaowatuma kwenu, naam, nikiondoka mapema na kuwatuma;…” Anarudia hapa: mara ya kwamza anasema hivi na anaongea kwenye mlango wa 26, na anarudia mlango wa 7 kuhusu kuondoka na mapema, na kuwatuma manabii wake, kuwaambia kile alichowaambia…na inasema, “lakini ninyi hamkuwasikiliza; Basi nitafanya nyumba hii kuwa Shilo”

Sasa angalia, unaweza kusoma hilo katika mlango wa 26. Na ndipo anaposema katika mstari 16, "Basi, wewe usiwaombee watu hawa…" Sasa hapa kuna tofauti kati ya ujumbe ninaoutoa leo na ujumbe Yeremia aliokuwa akiutoa huko nyuma: Mungu anatuambia sisi sasa hivi kuwa tunatakiwa kuliombea taifa hili. Inatakiwa tuombe kwa ajili ya kukosea, dhambi, uasi, uzinzi, ugonvi, uchafu, kuteleza, uovu, watu wapotofu sasa hivi. Lakini, kuna muda-maalum katika hilo-kama hawasikii, hapo Mungu anaenda kupiga vitu kiasi.

Sasa, nakumbuka nilitamka wazi wazi ule mstari mdogo ambao nimeusema sasa hivi, tulipokuwa tunaishi California. Hii ilikuwa kati kati ya miaka ya-80’s/mwanzoni mwa miaka ya 80’s wakati hii ilipotokea. Mungu alinitaka mimi na mke wangu kwenda San Jose, California. Tulikuwa Sacramento, na Mungu akasema: “Nataka uende pale ukatabiri juu ya San Jose”

Sasa, niliishi San Jose. Hapo ndipo nilipofanyia maisha yangu yote ya uasi—katika San Jose, California. Niliishi pale mahali nilipokuwa chuo pale, nilifanya dhambi zote. Ilikuwa katika uasi wa miaka ya 60’s. Hapo ndipo nilipoishi, na nilijua jinsi kulivyo na dhambi MAHALI PA LE PA WANAFIKI.

Hivyo, kwa vyovyote vile, alitufanya kuendesha gari kutoka Sacramento mpaka pale, na tukafika pale usiku wa manane. Tutateremkia mahali, nakawaza “ “Tunaenda kutabiti wapi?” Sawa, tukaishia kwenda kwenye kanisa kubwa lililoko pale. Nililifahamu kanisa lile nilipokuwa mwenye dhambi kwa sababu nilizoea kwenda pale wakati nimegongwa kichwa changu na dawa ya kulevya; Ningeweza nikaenda pale kuangalia jengo la kanisa lile kubwa.

Hivyo nikasema, “Ninakwenda pale”. Hivyo tukateremkia kwenye lile kanisa kubwa katikati ya mji. Kulikuwa na watu wengi kiasi {wakati mwingine}, lakini ilikuwa usiku, na hapakuwepo na watu wengi sana. Hivyo tukaegesha mbele ya lile kanisa na Mungu akalitoa neno lake, na bado ninalo bado lile neno likiwa limechapishwa----ambalo alisema ‘kwenda kuharibu San Jose katika muda wake kwa ajili ya dhambi zao”

Na tukalitoa neno, ilichukua kama dakika 10, na tukaendesha gari kurudi usiku ule ule --- kutoka Sacramento hadi San Jose, kutoa ujumbe, na kurudi. Tulifika nyumbani asubuhi sana, na wakati kila mtu alipokuwa akiamka, hapo tukaingia tukiendesha.

Lakini, tulipokuwa tunarudi, Mungu alitupa neno ndani ya gari yetu, na akatuambia kwamba alikuwa amekasirika, na alijilinganisha yeye na “mtu MLEVI. Ambaye huenda mezani, na kuchukua mkono wake na kugonga kila kitu mezani na kuharibu kila kitu”

 Sawa, mke wangu amekuwa akinieleza mara nyingi kwamba baba yake ambaye ni Mmarekani wa asili alikuwa kama hivyo: angeweza akalewa, akaja nyumbani kwa watoto wake baada ya kuvurumishana na wanawake wengine na amelewa usiku mzima, atakuwa mbogo. Atachukua mkono wake na kugonga kila kitu mezani kwa ghadhabu, na kulaani kila mtu pale…kwa sababu gani, sijui.

Lakini alikuwa akinieleza kwamba mara nyingi ndivyo anavyofanya. Na ni kweli, alifahamu haya yote, na nina uhakika ilikuwa dhahiri katika fahamu zake-baba yake mwenyewe alifanya hivi. Mungu anasema ni kama mlevi wakati amelewa; ana VUNJA KILA KITU JUU YA MEZA. Vema, hiyo ilikuwa mara yangu ya kwanza nilimsikia Mungu akitamka kuhusu Yeye mwenyewe anapokasirika kwamba anaenda kuwa kama mtu mlevi na kuvunja kila kitu mezani kwa ghadhabu.

 Ninalikumbuka hilo vizuri sana, hata leo hii. Ndiyo maana ninakuambia wewe kuhusu hilo. Na nimeiona hiyo ghadhabu katika Mungu mwaka uliyopita, na mwaka kabla yake.

Lakini, turudi kwenye mtandao. Kama ukienda kwenye mitandao hii, utapata kuona vizuri sana Mungu akigonga vitu kama mtu mlevi katika ghadhabu. Utaona magari yakisombwa, utaona magari yamelala kwenye magogo ya miti iliyoangushwa, utaona nyumba zilizofunikwa, na utaona kila kitu kidhaniwacho. MUNGU AMEFANYA HAYO NA HALI YAKE YA HEWA.

Hivyo Mungu hukasirika. Inabidi uwe nalo hili katika akili yako kuwa Mungu katika kanuni yake upendo, wa ya kweli atabasamupo uapoimba, na anapenda wakati unapopanga upya kila kitu kwa ajili yake, unapogeuza sura yake, unapobadilisha neno lake, unapotabiri uwongo, na kusema ni yeye kakuambia, kwamba unamkasirisha Mungu kweli. Na kuna upuuzi mwingi unaoendelea sasa---hao manabii hapo wanaojidhania hao ni manabii wanatuambia sisi “Hii ni kazi ya shetani; Mungu hayuko hivi; Mungu ni Mungu wa upendo…”

Na ni Mungu wa upendo, ni Mungu wa rehema, ni Mungu wa huruma. Kwanini unafikiri niliokoka? Alinirehemu nafsi yangu iliyoangamia wakati nilitakiwa nipelekwa Motoni---kwa ajili ya vitu nilivyofanya. Lakini, kuna wakati na majira katika Mungu ambayo inabidi tuyatambue, na tuko kwenye majira sasa hivi ambayo Mungu anasema: “Nimeleta uharibifu mwingi katika nchi hii”

Sasa, hebu tazama Marekani. Marekani ni haramu, rafiki. Marekani imevunjika. Rais wenu anatumia fedha nyingi kuliko zinavyoweza kuchapishwa. Tuna madeni kwa sababu ya “ahadi yake ya uwongo” hawezi akajitoa. Jeshi linafyonza isivyo kawaida na sasa linafanya ngono na wanyama, wanaobadili jinsi, ngono potofu, watu wa jinsi mbili, walawiti, wasagaji, wauaji, wabakaji, unaweza kuendelea; wapo jeshini sasa. Na wanapenda kuacha damu imwagike, ndio namna wanavyopata ashiki yao---wakati wanapoua mtu na familia yote katika vita --- wakati wakichukua dawa zao za vita na vitu vyote hivi.

Uchumi wenyewe umefilisika. Familia, wala siwezi kuliongelea hilo. Hakuna familia zilizosalia Marekani.Maombi hayapo tena shuleni, na utoaji mimba umeongezeka na kupewa kipaumbele kuliko vitu vyote duniani. Ulawili—mapinduzi ya pinki --- wanasonga mbele na kuna mashambuliza ya waislamu wakija kwa mamilioni sasa, wakialikwa na raisi wenu, wakimbizi wote kutoka nchi zote nyingine. Hivyo ndivyo nilivyoambiwa sasa.

Na nikamwambia mke wangu kabla sijazisikia habari hizi, kuwa asilimia ya hao watokao katika nchi hizo ambazo zimekuwa katika vita vile tulivyojihusisha navyo hapo, wengi wao ni WATU WA JIHADI chini ya mwavuli wa OBAMA AMETUALIKA HAPA.

 Kwa sababu gani? Hufikiri kwamba Mwislamu {Obama} ataruhusu fursa nzuri indoke? Na, kipindi hiki cha mpito, sasa, nakuambia kuhusu majanga dhahiri ambayo yapo tayari tayari sasa hivi hapa, na Waislamu katika taifa hili ni hatari kubwa ambayo isimgelipenda kucheza nayo. Ni vema ungerudi nyuma ukaenda kusoma historia ya Uislamu kama nilivyofanya. Utaona ni damu tupu kutoka mwanzo mpaka sasa---DAMU.

Na hapa tuna 9-11s mbili kabla hii ya tatu ya 9-11 hapa. Kuna 9-11s ambayo Waislamu walipoteza vita kubwa, na serikali ilifahamu hilo, hivyo wakamlaumu yule mtu wa tatu, ile 9-11 ya Waislamu, inayosema Waislamu walifanya hilo kulipiza kisasi kwa wale wengine 9-11 waliopoteza Ulaya.

Vema, hicho ni kitu ambacho yamkini hukifahamu. Yamkini unafahamu Waislamu hukimbilia sehemu hizo kwenye magorofa hayo na vitu hivyo vyote. Lakini hilo ni tatizo lako.

Lakini tukirudi nyuma katika hili, kuna mpiga mluzi katika Marekani, na ninamfahamu ni nani. Nilifahamu mambo yao kabla, na nimewafuatilia kwa miaka mingi. Wao ni wapinga-Uislamu; wanakupa tu taarifa za mara kwa mara. Wameshtakiwa na jamii ya Kiislamu karibuni. Sasa lisikilize hili: “kwa kufunua makambi yao yote ya mafunzo ya {mujahidina} kuzunguka mipaka ya Marekani”

Sasa, kama ukirudi nyuma kwenye baadhi ya makala zangu miaka 4, 5, 6, 7, 8 iliyopita---nilikuwa ninawaambia kuhusu haya makambi ya mafunzo. Wakati ule, yalikuwepo 8 au 9 ambayo niliyafahamu katika majimbo mbali---ninaongelea kuhusu makambi ya mafunzo ya mujahidana ambapo kulikuwepo na 100S YA MAFUNZO YA WAISLAMU YA KUICHUKUA NCHI HII KWA GHARAMA YOYOTE.

Na baadhi ya watu wakubwa katika hizo nchi za Kiarabu wanayasaidia kwa mabilioni ya dola, na hakuna wasiwasi kwamba rais wako mweusi ni mshirika na watu hawa, wakati walipokuja kama wakimbizi kutoka katika nchi hizo. Hili lilifunuliwa na vyombo binafsi vya habari, na sio kikundi chenye njama, bali chombo cha habari kililiweka tu hili hadharani hapa siku chache zilizopita, kwamba Obama amekuwa akiyafanya haya. Ilinukuliwa nyuma wakati Obama alipokuwa akiwatumia baadhi ya watu hawa, wajulikanao kama Mujahidina kutoka katika nchi hizi. Na hakuna mashaka amekuwa akituma na kufadhili watu hawa katika makambi haya ya mafunzo. Wakati akitaka vita vya ndani, atakachotakiwa kusema tu ni “Saa imewadia”

 Hivyo, kama Mungu anataka kutumia tishio hilo, Mungu atatumia tishio hilo. Kitu ninachojaribu kuwaeleaza, watu, ni kwamba tumekalia bomu abalo linaweza kulipuka saa yeyote Mungu anaposema linaenda kulipuka, na NI MUHIMU KWAMBA TUKAOMBA KWA AJILI YA TOBA, kwa angalau baadhi ya watu waokolewe. Wala simtafuti Mungu aondoe mkono wake wa hukumu kwa Marekani----kwa sababu sidhani kwamba Marekani, kama taifa litatubu. Lakini ninaamini, na Mungu amesema, kuwa kutakuwa na baadhi katika nchi hii ambao wataona makosa ya njia zao, na kutubu, na kuwa sawa mbele za Mungu. Lakini , kama taifa, halitafanya hivyo. Na ninaamini kwamba saa inakuja, na nimekuwa nikisema hili kwa miaka, kwamba Mungu ATAITEKETEZA MAREKANI.

Analia, Ujerumani ilitokomezwa, Urusi iliteketezwa, Hispania iliteketezwa, na Uingereza ilikaribia kuteketezwa. Nina maanisha urudi nyuma kwenye baadhi ya hivi vita katika karne ya 18 mpaka ya 14, 15, na 1600’s, katika enzi hizo, utakona kulikuwa na uharibifu mkubwa. Na mwingi kati ya uharibifu huo ulisababishwa na Waislamu na Watoliki wa Roma; walikuwa tishio. Sasa, unalifurahia hilo

Sasa, tunarudi nyuma kwenye Shilo. Ilinibidi kuanza na kikwezo cha msemaji barabarani kuhubiri hapa kuhusu mstari wa 16: “Basi wewe usiwaombee watu hawa,” na nilikuwa ninasema kuna tofauti kati ya wakati huo na sasa.Mungu aliwaambia “Basi wewe usiwaombee watu hawa,…kwa maana sitawasikiliza. Wamepitiliza muda wangu wa mwisho”

Hayo ndiyo ninayojaribu kuwapatia ninyi watu: tumepewa muda. Sasa hivi tunatakiwa tufanye maombezi, lakini iko siku itafungwa, na ndipo Mungu atatuambia, “Basi msiombe tena. Ninaenda kuteketeza”

 Ni nini kilitokea Shilo? Vema, tunafamu Israel walikuwa wenye dhambi. Tunafahamu makuhani walikuwa wakitenda dhambi; tayari tulifahamu yote waliyokuwa wakiyafanya. Vema, ni nini kilitokea pale, mpendwa, ni Wafilisti walilichukua sanduku la Mungu la agano kutoka nchini kwao miezi 7. Ilikuwa kama ni kuuiba moyo wa Mungu na kuupeleka katika nchi ya kipagani….kulinajisi.

Sanduku la agano liliwakilisha uwepo wa Mungu katikati yao, na liliibwa huko Shilo kwa sababu ya dhambi zao---sanduku ka Mungu mwenyewe. Neno lake lilikuwepo pale. Na vitu vingi vilivyowakilishwa pale: Nguvu zake, Uwepo wake, kila kitu kiliwakilishwa pale kwenye sanduku la agano; likachukuliwa na adui. Hudhani kuwa adui ataweza kuchukua moyo wa Marekani na kuunajisi? Sawa, lile hema la kuabudia pale Shilo ambapo sanduku la agano lilikuwa huko, na watu walikuwa watenda dhambi, na Mungu akawatumia hawa wafilisti wapagani---waliabudu miungu mingine, na kufanya uchafu mwingine wote---wakaingia, na hawakubakiza Shilo, wakalifanyia lile sanduku vituko katika ghadhabu yao; na GHADHABU YAO ILIKUWA GHADHABU YA MUNGU. Vema, tunafahamu historia, hebu turudi pale. Ujumbe wangu, leo, ni katika 1Samweli mlango wa 7.

Sasa, mlango huu mzima wa 7, mstari wa 1 hadi wa 17 unazungumzia kile ninachokizungumzia. Sweli alikuwa nabii, NI nabii wa Mungu wa siku hizo. Na hatimaye katika mstari wa 3, hapa ni nini kinatokea: Basi Samweli akawaambia nyumba yote ya Israel, akasema, “Ikiwa mtamrudia Bwana kwa mioyo yenu yote, basi, iondosheni mbali miungu migeni, nayo Maashtorethi yatoke kwenu, mkamtengenezaa Bwana mioyo yenu, mkamtumikie yeye peke yake; naye atawaokoa katika mikono ya Wafilisti.”

Sawa, hawakuchukua tu sanduku la agano, lakini Wafilisti kadhalika walifanya vita dhidi ya Israel, nao walikuwa wamepagawa---kwa sababu wakati moyo wa Mungu ulipochukuliwa katikati yao, hiyo iliwadhoofisha sana. Haikuwa dhambi zao peke yao, lakini kulipoteza sanduku la agano iliwafedhehesha. Hiyo ingekuwa kama China kuja hapa (Marekani) na kuwafukuza watu wote mjini na kuweka bendera yao Nyekundu ya Kichina mahali bendera ya Marekani ilipokuwa iankaa; huo ndio moyo wa Marekani. Unaweza ukalifikiria hilo?

Au kuhusu Uislamu? Uislamu ulishasema kwamba wanakuja kufanya hivyo. Wamekwisha kuja wanakwenda “kuchukua bendera ya Marekani iliyoangamia na kuitupa chini na kuichana, na kuiunguza” nao “wanakwenda kuinua bendera yao ukiwa na upanga juu yake, na itaenda kupepea katika nchi hili, pale pale katikati ya nchi hii, katika Washington D.C.” Majengo ya mji mkuu peke yake ni sanduku ka Mungu la agano kwa taifa hili.

 Tayari wamekwisha dai hilo. Wamekwisha sema wanakwenda kufanya hivyo. Ndiyo maana majahidina wako hapa, ndiyo maana wana kambi za mafunzo, ndiyo sababu Obama anawaleta watu, ndiyo maana wanafanya kile wanachokifanya, na Mungu hazuilii chochote. Na mara nyingi nimejisemea mwenyewe, “Kwanini FBI wasiende pale? Kwanini polisi wasiende pale? Kwanini jeshi lisiende pale na kuwazuia watu hawa? Wanafahamu wako hapo”.

Hakuna neno lililozungumzwa kwenye vyombo vya habari---hakuna hata neno moja---miaka yote hii ambayo nimesoma, isipokuwa sasa hivi. Na hawakuwa wanaongelea kuhusu haya makambi ya mafunzo, zaidi ya kesi za mahakamani. Na sasa, tovuti yao imeondoka kabisa; kama ukuangalia kwenye tovuti yao ambayo inatamka yote haya, imekwisha ondoka kabisa. Niliiangalia siku moja, haipo. Wamewafanya waiondoe.

Kuna Waislamu wameanikwa wazi kwamba wana kambi za mafunzo za kuharibu Marekani hapa hapa katika nchi hii, hapa hapa. Na moja kati ya kambi yao kuu iko New York, katika milima ya Catskill. Naifahamu fika mahali ilipo katika ramani kwa sababu nimesema hayo muda mrefu---hiyo ni moja ya ofisi yao kuu.

Na wanawafunza watu hawa kama jeshi maalumu kwenda na kuua kikatili yeyote na kila kila mtu---wakati muda utakapotangazwa. Na hawa watu walikuja na kuwashtaki watu hawa ambao waliwapulizia mluzi; waliondoka nayo kwa sababu tovuti yao haipo, nao wanashtakiwa kwa kufanya hivyo. Umeshasikia watu wakiulizia? Hakuna anayeulizia. Unafahamu ni kwanini? WATU WAMELALA NA WANAKOROMA. WALA HAWAITAMBUI HATARI ILIYOPO KATIKA TAIFA HILI.

Nakuambia hivi, rafiki: kwa jinsi ulivyo mkatili mbele za Mungu, Mungu anaweza kukugeuzia watu wakatili dhidi yako. Alifanya hivyo kipindi na kipindi tena, Amefanya hivyo kwa jinsi historia inavyoonyesha, na atafanya hivyo kwa taifa hili. Kama hutatubu dhambi zako, na kama hutamrudia Mungu---kuweka moyo wako sawa, na kuiondoa miungu yako migeni---Mungu anaweza kukugeuzia hawa watu wakatili dhidi yako. Wanaichukia nchi hii, wanawachukia Wamarekani, sasa sana wanawachukia wakristo zaidi. Watakuwa na rehema sufuri ----katika umwagaji wao wa damu---kama Mungu akiruhusu; na yamkini, Mungu anaweza akaliruhusu hilo.

Sema,“Sawa pllisi watatulianda---serikali itatusaidia” Serikali inawasaidia…Hiki ndicho ninachojaribu kukueleza wewe. Ni lini Taarifa za ABC zilisema Obama alipatikana na hatia ya kutumia hawa majahidina---akiwaleta hapa kwa siri katika uhamiaji wa watu hawa wanaokimbia katika nchi hizo, anafanya nini na watu hao? Anawapa misaada kwa kutumia hizi kambi za mafunzo. Nimeongeza hapo kwa sababu najua ni kweli.

Yeye sio Mkristo. Ana agenda ya kisoshalisti na kikomunisti, yeye amapenda Uislamu kwa siri, na anafanya kila kitu kilichomo kwenye uwezo wake kuulinda Uislamu na chochote anachoweza kukifanya kuuharibu Ukristo katika nchi hii. Kwa hiyo kama una muunga mkono Barrack—Barry, Barry mwongo— ni heri ungetubu kwa hilo. Huyo mtu ni pepo. Hebu nirudie hilo:YULE MTU NI PEPO KATIKA MWILI WA MWANADAMU. Hayuko kitu kama hicho?

Sawa, turudi Shilo. Sasa, liangalie hili. Kwanza kabisa, TUBU. Geuka; tubu mbele za Bwana. “Hilo ndilo Samweli alilosema unalotakiwa kufanya” Namba 2, mstari wa 4,

‘Ndipo wana wa Israel wakawaondoa Mabaali na Maashtorethi, wakamtumikia Bwana peke yake.” Walitubu. Waliamriwa watubu; wakatubu na sasa tunaona hapa katika mstari wa 13: “Hivyo Wafilisti wakashindwa.” Maadui walishindwa. Sasa, mpenzi, hiyo ndiyo rasimu. Sasa hivi, wito wa toba umetolewa na watumishi wa Mungu, na umetoka ----“TUBU.;TUBU.

 Na sasa tunasubiri kusikilizia. Tunatubu, na tungependa kuona matunda yapasayo toba. Sitaki kuona mwanga uliofifia, na muziki laini ukiimba na vichwa—vyote—vimeinama! NATAKA NIONE TOBA. NATAKA NIONE WATU WAKILALAMA, WAKIUGUA, WAKILIA KWA AJILI YA DHAMBI DHIDI YA MUNGU. NDIPO NITAKAPOAMINI.

Sitaki kuuona huu upuuzi wa Billy Graham unaouona wakati watu wanapoinamisha vichwa vyao na kufanya kana kwamba wanatubu, kwa maana mara watakapoinua vichwa vyao, wanakimbilia kwenye madanguro. Huu ni ukanisa wa BabeliI katika watu---wala hawatambui ni nini maana ya “toba”. Toba maana yake ni kugeuka; kwa kweli, kugeuka na kurudi ulikokuwa unakwenda. Hiyo ndiyo maana yake---KURUDI ULIKOKUWA UNAKWENDA. "Sawa, Mungu ataniokoa mimi katika dhambi zangu” Hapana hatafanya hivyo; siku hizo zilikuwa tamu sana; kuna muda uliowekwa kwenye hili suala la toba.

 Na kama tukiendelea kulilia watu watubu, wala haitoshi, Mungu atasema “Usiwaombee tena watu haoNafahamu muda huo utawadia kwetu. Najua Mungu atasema “Hapana, hawasikii.Hawajatubu; acha kuwaombea. Sasa ninakwenda kufanya oporesheni yangu ya kuteketeza”.Naamimi Mungu ataenda kufanya hivyo---kama hakuna toba ya kutosha.

Sasa, ninaamini anaenda kufanya hivyo kwa vyovyote, lakini anatoa muda wa kutubu, amesitisha tu kwa muda, ili watu wakae sawa na Mungu kwa sababu anakwenda kuwashinikiza wakae sawa na Mungu. Lakini kama taifa, sio sasa, wala sihitaji mtaalamu wa hali ya hewa kunionyesha upepo unakoelekea: unakuja tu---kwa maana nchi hii, inakiu ya kumwaga-damu. Na nchi isipotubu, ikatubu kwa ajili ya utoaji mimba, kutubu kwa ajili ya mauaji yake ya vita, na uvamizi ambao imekuwa ikifanya kwa miaka nenda rudi, hakuna matumaini kwa taifa hilo isipokuwa DAMU katika mahali hapa.

Na Mungu alituambia, wala sijali kukuambia kadhalika. Mungu alituambia iko siku tutaona damu ikimwajika mitaani Marekani inayofikia kwenye magoti. Alitueleza nyuma kipindi tulipokuwa Montana, wakati tulipokuwa wakristo wachanga katika suala hili. Alisema, “Siku zinakuja katika nchi hii ambapo mtaona, kwa macho yenu wenyewe, bamu ya kufikia kwenye magoti ikitembea katika mitaa ya Marekani”

“Sasa, huo waweza kuwa mfano." Mungu hutumia mifano ili tuelewe, labda sio kama hivyo, lakini inategemea kama wewe ni mtoto mdogo, wala sio juu sana. Kama urefu wako ni inchi 6' 8" mcheza mpira, hapo kidogo inaweza kuwa nyingi. Lakini, mfano ulikuwa “kufikia magotini” Hiyo inatosha kunifedhehesha---mitaani Marekani damu itakuwa inatembea.

Sawa, “tubu”. Wakatubu. Ndivyo inavyosema, “Hivyo Wafilisti wakashindwa, wasiingie tena ndani ya mipaka ya Israeli na mkono wa Bwana ulikuwa juu ya Wafilisti siku zote za Samweli. Na miji ile Wafilisti waliyokuwa wamewapokonya Waesraeli ilirudishwa tena kwa Israeli.”

Unataka Marekani irejeshwe? Unataka zile siku nzuri za zaamani zije? Unataka amani nchini? Unataka hawa mashoga na hawa majahidina watoke katika nchi hii? Je, unataka ukomunisti uondoke?

TUBU DHAMBI ZAKO, KAA SAWA NA MUNGU, ACHA KUABUDU MIUNGU MIMGINE, NA MUNGU ATAFANYA KITU KWA TAIFA HILI. WALA HAIHITAJI KILA MTU KUFANYA HIVI. WENGI WANAWEZA KUBADILISHA HISTORIA YA TAIFA HILI; WANAWEZA WAKABADILISHA NIA YA MUNGU---KAMA WANGELIFANYA HIVYO.HIVYO, SASA TUKO KATIKA MUDA WA MAPINDUZI YA TOBA. AMEN.

 JE, UMEKWISHA OKOKA? YESU NI HALISI!! OMBA KAMA HIVI.

Mpendwa Yesu, ninakuja kwako na dhambi zote nilizozitenda na ninakuonba wewe unisamehe. Niokoe mimi kutoka kwenye maangamizo ya milele katika moto wa Kuzimu. Ninakiri kwamba mimi ni mwenye dhambi ambaye siwezi kujiokoa mwenyewe.Usiniruhusu mimi nife katika dhambi zangu. Tafadhali takasa mwili wangu, nafsi na roho kwa damu yako ya thamani.Ninahitaji msaada wako na ninakuomba wewe uje na kuishi moyoni mwangu. Nataka nikutumikie, kutii amri zako na kufanya yale ambayo ni sawa. Nataka niishi kwa ajili yako kila siku na kuupokea uzima wa milele.Tafadhali niongoze na nielekeze kwa Roho wako katika haki. Nisaidie mimi kuishi maisha safi na matakatifu yampendezayo Mungu. Asante Yesu kwa kunisikia na kunijibu maombi yangu. Amina! Soma BIBLIA!

Tuandikie kwa ajili ya kupata bure machapisho yetu mengine yanayohusu HUKUMU YA MUNGU.

Tungependa kusikia kutoka kwako!
Kuomba maandiko au taarifa zaidi kuhusu sisi au jamii yetu tafadhali tutumie E-mail:

livingword@aggressivechristianity.net

 au tuandikie:

AGGRESSIVE CHRISTIANITY
HR 60, Box 11,
Fence Lake, NM 87315


Kwa maelezo zaidi kuhusu ACMTC TANZANIA, au jinsi utakavyoweza kujihusisha, wasiliana na Meja Frank & Elina Materu: S.L.P. 7579 Dar es Salaam, Tanzania. Barua pepe: materufrank@yahoo.com