Home || The Aggressive Vision || Prophetic Word Of The Lord || On Line Library || Current Articles and What's New
Free Literature || Visions from The Lord || More About ACMTC || Contact


Wakati Ujao

(Sehemu ya 1)

Gen. Deborah Green

BWANA ASIFIWE. Karibu kwenye Mlio wa Vita/ Mshindo wa Mlio wa Vita. Na bunia ninini? Bwana yuko kwenye mwendo anatembea.

Unajua, Bwana anatutaka tukaze macho yetu kwake; ni rahisi kwa Wamarekani kuweka macho yao kwenye siasa. Sasa je sio kweli? - Kumkazia macho yao yule aliyeko kwenye nyuma ya wale wenye mrengo wa kushoto, ambao hufanya hivi na kufanya vile na kujifanyia wenyewe kila kitu tayari, hujikusanyia vitita vya chai, na kufanya haya matamko makubwa kwamba ondoka, na uache haya maonyesho yote makubwa na majigambo na yote hayo.Lakini unajua, hilo sio jibu kabisa. Jibu ni TOBA, na kwa kupitia MUNGU ALIYE HAI, na jibu ni katika kutembea sawa na kuweka macho yetu tukimwangalia Yeye.

Sasa, unajua, siku za karibuni nimetoa tamko, kwamba mimi sipo chini ya uchungaji wa yule asiyestahili kuheshimiwa ‘mheshimiwa mchungaji’ Joey Osteen. Nilisema "YEYE SIO MCHUNGAJI WANGU"—kwasababu vombo vya habari vimetungwa kwamba yeye ni "Mchungaji wa Marekani." nilisema, "YEYE SIO MCHUNGAJI WANGU, NA MAREKANI SIO NCHI YANGU, LAKINI MIMI NI RAIA WA UFALME WA MBINGUNI.”

Je, unajua kama Wakristo wote wanatakiwa raia wa ufalme mbinguni? Je, unajua kwamba tumeruhusu udanganyifu wote huu wa kizalendo ututenge na Mungu? Mungu hajawahi kusema tuabudu nchi; hajawahi kusema tuabudu taifa; hajawahi kusema tuabudu viongozi; hakuna hata mojawapo ya hayo aliyowahi kusema. Hiyo yote ni adhari kubwa ya sanamu ambayo inajiingiza ndani, na Wakristo sasa wanadhani wanatakiwa kufanya hivyo.

Unajua, Wakristo wengi hupiga kite na kugumia kuwa tunapoteza hiki na tunapoteza kile na tunapoteza hiki na wanajaribu kabisa kujipotezea kwenye krismas, na ndicho wanachoenda kukifanya hapa, vivyo hivyo pale na unajua ni kwanini? Ni kwasababu WAKRISTO HAWAACHI SANAMU ZAO, sasa Mungu anawaachilia Wa-ashuru watudhihaki kutokana na hilo. Na hata waziondolee mbali nasi sanamu zetu – sio Waashuru peke yao tu bali hata mataifa mengine yaliyo maovu kwenye ulimwengu wa roho. Lakini mbali ya hayo yote, hebu tuingie kwenye mada yetu ambayo ni “Wakati Ujao”

Sasa, leo ni Januari 1, 2014, kwahiyo ni siku nzuri kiasi gani ya kusikia mambo ya wakati ujao! Sina mpira wa fuwele, sina majani ya chai chini ya kikombe, wala siendi kutazama kiganja cha mkono wangu, lakini nitaenda kuwaeleza kuhusu mambo ya wakati ujao. Kwanini? Kwasababu neno la Mungu hutupatia muktasari, wa mbeleni—kama kweli tutamfuata Bwana.

Sasa, tunakwenda kwa Marko sura ya 13, na nitakuwa nasoma tafsiri ya Biblia ya Amplified. Pia, yako maandiko yanayofanana na hilo kwenye Mathayo 24, na naamini pia yako ya hivyohivyo kwenye Luka 21. Lakini leo tutakazia kwenye Marko, na tutaanzia hapa kwenye mlango wa 13, mstari wa 1.

Na inasema, "HATA [Yesu] alipokuwa akitoka hekaluni, mmoja wa wanafunzi wake akamwambia, mwalimu, tazama, yalivyo mawe na majengo haya!" "Angalia Mwalimu, angalia kile tulichofanya; angalia vile mtu anavyoweza kufanya; angalia maendeleo makubwa yaliyoko hapa, mafanikio makubwa ya hapa; angalia kazi kubwa mwanadamu anazoweza kufanya. Ninamaanisha yaangalie mawe na majengo haya" Sasa, hawakuwa wametengeneza mawe yao wenyewe, siamini; lakini, yale mawe bila shaka yalikuwa yamechongwa vyema ili yawe ya ukubwa unaotosha katika umbile la jengo, hayo yalikuwa yalikuwa ni yale bora tu: "Yaangalie majengo haya!"

"Bwana alinipa maono usiku, ya kujenga majengo kwa ajili ya Bwana, yalitakiwa kuchukua eneo la eka10. Sasa unaweza kuwa sehemu ya kazi hii kama ukitaka kutuma leo dola $99.95, halafu jina lako litawekwa kwenye orodha, na utakuwa sehemu ya wajenzi wakuu” Je, Mungu hujali juu ya majengo yaliyojengwa ya eke 10? Eeeh eh; la hasha; hapana, hizo ni kazi za wanadamu.

Kwahiyo, alikuwa anasema, "Hei mwalimu, angalia hapa na angalia kile tunachoweza kufanya" kulizoeleka kuwepo kitabu cha watoto wadogo, na vitu hivi vilikuwa, "Sasa wameniweka kwenye bustani ya kufugia wanyama pori na tazama kile ninachoweza kufanya; naweza kufanya hivi na naweza kufanya vile.” Wasanii wengine, unajua, wangeweza kufanya vikorokoro vyote hivi. Na kwa uhalisia ndivyo huyu alivyoonekana kwa Yesu.

"Hei mwalimu, angalia, hei tazamaa, tazama kile tulichofanya, angalia hiki!" kana kwamba Yesu alikuwa HAJUI kitu kuhusiana na lile hekalu. Namaanisha wote walikuwa wanalifahamu. Ni kama vile NI kitu kilichozungumziwa zaidi, bila shaka, na kitu walichojigambia zaidi, na kilichokuwa MAFANIKIO YAO MAKUBWA ZAIDI.

Sawa, na maanisha ningeweza kuelewa kwa niaba ya Wayahudi – kwa kuwa uasi wao wenyewe, na kuabudu kwao sanamu, na kwa maovu yao yaani yamepunguzwa na kuwa rundo la kifusi. Lakini, cha muhimu hapa ni kwamba, tunakwenda kuona jinsi Yesu alivyojisikia kuhusiana na majengo yao, na kuhusiana na mawe yao na kuhusiana na mafanikio yao na kuhusiana na kazi zao.

Akasema, “Na Yesu akamwambia, wayaona majengo haya makubwa? Halitasalia hapa jiwe juu ya jiwe ambalo halitabomolewa." Je wewe huoni pande la mchungaji mwenye kanisa kubwa? Ambaye amejenga kanisa kubwa, na anatembea tembeatembea akitaka kila mtu ajue “huu ni usiku wa tunaokwenda kuweka jengo hili wakfu kwa Mungu.” Na neno la Mungu linatoka kwa nabii wa kweli wa Mungu likisema." Eeh, eeh, eeh kabla mwaka haujaisha, jengo lako litakuwa rundo la kifusi."

Sawa, kitatokea nini? Kwanza kabisa, watamfunga mikono huyo nabii wa kweli, wataweka tambara mdomoni mwake – ili asiweze kuongea tena maneno ya kweli na kwa haraka watamburuza nje na kujaribu kumweka gerezani milele –kwasababu amenena kinyume na jengo kubwa. Lakini tena sikiliza kile Yesu anachokisema. “Na Yesu akamwambia Wayaona majengo haya makubwa? Halitasalia hapa jiwe juu ya jiwe ambalo” nini? Ambalo halitabomolewa."

Kwa hiyo anasema nini? Anasema, "Jengo hili lililokamilika kwa ustadi mkubwa, mafanikio haya makubwa, maonesho haya, hayana maana yoyote kwangu, na hayamaanishi chochote kwa Mungu. Ni kitu chenu, ni kitu chenu."

Kwahiyo, analifafanua – kwamba hajengi kwa namna njia ile waliyojenga. Kwasababu alifanya nini? Alikuja kuanzisha utaratibu mwingine, sasa kwanini anahusika na utaratibu wa zamani? Kwanini anakwenda kuheshimu utaratibu wa zamani na kusema, "Sawa tunapaswa kuyatunza kwakuwa ni majengo ya kumbukumbu ya kihistoria na yanaweza yakaja kumaanisha kitu fulani wakati fulani. Na tunatakiwa kuyatunza….kwasababu yanawakumbusha watu wa Uyahudi historia yao….na mmmh….. tunapaswa kuyatunza kwakuwa tunatakiwa kuwa na mahali….kuhifadhia mambo ya dini…kuyahifadhi kwa raha katika utaratibu wake na desturi ileile”? hakusema hata mojawapo la hayo. alisema, "yote yatabomolewa."

Ulishafahamu kuwa hayo ni mapinduzi, na ulishafahamu kuwa hicho ndicho Mungu anachokitaka kwenye maisha yetu, na ulishafahamu wakati tunapotubu, tunatakiwa kumruhusu mjenzi mkuu ayaangushe chini majenngo mengine katika maisha yetu – ili aweze aweze kujenga jengo lake katika maisha yetu? Ili tuweze kuwa hekalu lake, ILI TUWEZE KUWA HEKALU LAKE?

Tunatakiwa kuwa mawe yaliyo hai. TUNATAKIWA KUWA BARUA ZILIZO HAI. – TUONEKANE NA KUSOMWA NA WATU WOTE. Kwa maneno mengine, tunatakiwa kumruhusu Kristo aumbike ndani mwetu – katika kiwango kile ambacho watu watatuangalia na kujua kwamba sisi ni wa kwake. Sawa kabisa na vile walivyokuwa wanafahamu kwamba lile hekalu lilimaanishwa kumwakilisha Mungu yule ambaye walikuwa wakimfuata kwanzia siku zile za jangwani – baada ya kuivuka bahari ya shamu – ambapo walimfuata, sio kwa uaminifu, sio kwa imani, sio kwa uadilifu, lakini kwa kudhaniwa. Halafu wakawa wakijivunia hekalu lao kubwa, lakini tunatakiwa kumwakisi Kristo ndani yetu, tumaini la utukufu.

Tunamaanishwa kutembea katika mchakato wa kufanywa kuwa katika sura na kumfanania Mwana wa Mungu. Hivyo ndivyo hatima yetu ya baadaye inavyotakiwa kuwa. Sasa, unaangalia malengo, yale yaliyokwishafanyika, vitu ambavyo watu hutafuta kutambulika kwavyo katika ulimwengu wa kidini, “Sawa ninavyo vingi sana katika dhehebu langu." "Sawa, tumejenga makanisa mapya matano." "Hah! Sawa, unadhani wewe ni chochote? Sisi ndio kwanza tumejenga makanisa mapya 50." "Hah!? Sawa, unadhani wewe una kitu chochote; unatakiwa uone JENGO LETU. Jingo letu linauwezo wa kuhhimili kimbunga, tornado, kuzuia moto, kumzuia Mungu, hakuna chochote kinachoweza kuingia ikiwa ni pamoja na mwanadamu mkubwa." "Wuu! Nyie watu mmeyapata kwa pamoja, hayo yote mmejifunza wapi?" “KUTOKA KWA SHETANI.”

Sasa angalia, tutazame uhalisia. Kanisa la kisasa linajihusisha zaidi na vitu vya asili, vyenye udhihirisho unaoonesha KAZI ZAO kuliko kuliko kitu chochote cha kinachohusu kazi ya Mungu. Sasa, je, hiyo ni kweli? Eeeh ni kweli. Kwahiyo, Mungu hututaka tuwe kwenye hali hiyo? Kwahakika hapana. Je, Yesu alisema hatima ya wanafunzi wake wa ukweli ndivyo itakavyokuwa? Hakusema hata neno moja la hayo.

Ninapata barua hizi na watu wanasema, "mimi ni mpanda makanisa." nawaza, "nionyeshe basi yalipo ili niweze kuja na kuyang’oa" "mimi ni mpanda makanisa." Unajua, watu husema, "nioneshe kwenye maandiko kitu chochote kinachohusu Mungu kutaka jeshi!"

Sawa, nionyeshe katika maandiko kitu chochote kinachohusika na Mungu kutaka wapanda makanisa. Sawa, unadhani kwa vile unatumia neno, "kan…isa" …wala siendi kulitamka neno hilo baya; unaddhani ukitumia neno k….n...s, hilo linakuweka katika msimamo mzuri na Mungu. NI BORA UIPIME TENA THEOLOJIA YAKO. KAMA UKITUMIA NENO “K-N, NI KWAMBA UNAMKASIRISHA TU MUNGU. Kwa vile huo hujawahi kuwa mpango wake. Huo haukuwa utaratibu wa Mungu. Hilo sio jengo la Mungu.

TU-memaanishwa kuwa mahekalu. Kwahiyo, je, nahitajika kukimbia duniani mwote kutoa hela ili makanisa yajengwe? Hapana. Kama mimi ni mjumbe halisi na chombo halisi cha Mungu, ninamaanishwa kuujenga mwili wa Kristo kwa wanachama hasa. Sawa? natakiwa kuwalisha, natakiwa kuwaelekeza, kuwaongoza, kuwaonyeshea – kama vile Mungu alivyonifanyia.

Sasa, je, hivyo si ndivyo Paulo alivyosema? "Nifuateni mimi kama nami ninavyomfuata Kristo." Kwa maneno mengine, "nimemruhusu Kristo anishughulikie, sasa na wewe mruhusu akushughulikie – ili uweze kusogezwa mbele katika kile Mungu anachotaka kwako."

Sasa hebu nirudi nyuma hapa kwenye andiko letu, na kwa habari za wakati ujao kwa kuwa kweli tunatakiwa kujua habari HATIMA yetu; leo ni siku kuu ya mwaka mpya. Sawa, kwahiyo tunaona kwamba ni Yesu anasema, "unajua nini, yote haya yanakwenda kuporomoshwa chini."

Sasa, nakwenda kuingia kwenye jambo hapa ambalo Marekani inatakiwa kulitubia – Wamarekani wanaojiita Wakristo. Kile walichokuwa na ufahari nacho sana katika hekalu hili, Kile walichokuwa na ufahari nacho sana katika majengo haya makubwa, Kile walichokuwa wakitaka sana akitambue ni UFAHARI wao,…majigambo yao.

Sawa, majigambo ya mfumo wa maisha. "Sawa kwa hakika tunalo hekalu lililojengwa kwa ubunifu wa hali ya juu tunaloweza tukalitumia. Je, unajua katika maliwato ya kike kuna kioo kinachogharimu dola 50,000 na kitu hicho ni kirefu sana kinaanzia sakafuni hadi inakoanzia dari - sehemu ya kuogea? " Nani anajali? Panatakiwa kuwa chumba kilichowazi mahali ambapo unakwenda ku foo-foo na niii zako, kisha ukajijazie vipodozi vya siagi usoni mwako – vya rangi mbalimbali na hata vipande vidogodogo vya vioo vinavyoweza kukata na mchanga?

Je, unajua rangi ya macho maarufu kama eye-shadow zinavioo vinavyokata ndani yake—kwa wale mnaotaka kutazama kama vile mna macho meusi. Unataka macho meusi, ingia tu kwenye mapambano na mumeo; atakutunza. Hapana, bora ujiwekee vioo vinavyokata juu ya macho yako – kama baadhi ya makahaba wa Misri….."Wakristo."

Na halafu unataka kuweka krim kubwa, nene, na ya zamani kwenye midomo yako – ambayo itakuwa ikidondoshea rangi kwenye meno yako unapoongea. Na kisha unapokula, yote inayeyuka na kutiririka hadi kwenye kidevu chako. Na hatimaye mwisho wa siku, ulichokipata ni michirizi ya hicho kitu, halafu kile watu watakachooona ni nikwamba ulikuwa ukijaribu kuifanya midomo yako ionekane mikubwa, na kuinyanyua juu pale; ni kweli.

Kujipodoa – unatakiwa kuwa na kioo cha kujipodolea. Je, unajua kama wanaviuza vitu hivyo? ….. vina taa kubwa za kuvizunguka. Wanaviita vioo vya kujipodolea. Unafahamu kama wanawake wengi hupata ajali za ghafla kwasababu ya kujipodoa wakati wakiwa wanaendesha gari kuliko sababu nyingine zozote?

Sawa, kiburi cha mtindo wa maisha, kiburi cha kazi, kiburi cha majengo. "Heh, mwalimu angalia hapa, angalia kile tulichofanya." akasema, "unajua ninini ninachokiwaza juu ya kile mlichofanya? Yatasambaratika” SAWA, DHAMBI MOJAWAPO KUBWA YA WAKRISTO WA MAREKANI NI NINI? – KIBURI CHA MITINDO YA MAISHA.

Ah, asubuhi ya leo nilikuwa nawaza juu ya hili wakati Bwana alipokuwa akinihudumia. Na unajua, walikuwa na hiki kinachoitwa filamu za “Wakristo” ambazo zimemaanishwa kutoa na kuweka kanuni. Filamu zote zinafanana.

Kama asemavyo mume wangu, ‘Mara zote wanakuwa na wanawake wazuri, wenye meno timilifu, umbo timilifu na nguo nzuri. Mara zote wanakuwa na mwanaume aliyekaliwa na mkewe ambaye mambo yote ya familia kwake yako ovyo. Kisha mara zote unakuwa na nyumba NZURI maridhawa yenye samani zote, au nyumba imilikiwayo kwa shirika, au vyumba vya kuishi, lakini mara zote inakuwa nzuri sana – haiwi hata na unyoya mmoja wa mbwa, haina hata alama moja ya makucha ya paka kwenye hizo samani, hakuna kitu chochote ambacho hakiko mahali pake, kila kitu ni maridhawa, uzuri wa viwango vya juu. Mtu anakuwa akijipatia hela nyingi, au kitita au pochi yote imejaa noti – kwavile unazungumza kuhusu mambo yanayohusu vyombo na vikorokoro” yaani kiburi cha mitindo ya maisha

Kitu cha kwanza wamisionari wanaoenda dunia ya tatu wanachotaka kufanya ninini? Wanataka kupandisha viwango vya mitindo ya maisha ya watu. Sijasoma hata mara moja mahali ambapo Yesu alisema “mnatakiwa kupandisha viwango vya maisha” Sijasoma hata mara moja mahali ambapo Yesu alisema “vitu na vikorokoro vyenu vinaonyesha mnanipenda”

Sijasoma hata mara moja mahali ambapo Yesu alisema “uzuri wenu na namna mnavyobembelesha vitu vyenu viwazungukavyo na aina ya gari mnaloendesha, na namna vile unavyokaliwa na mke wanu, Ahabu, na endelea, na namna ile Yezebeli anavyotawala kwenye himaya na haachilii hata inzi atue kwa dakika moja …. Inaonesha kweli unampenda Mungu.”

 Na mchoro wenyewe ni hafifu sana. Siwezi hata kuutazama. Wala Mungu hataki niutazame. Ni upumbavu. Ni kama magazeti yale madogo uliyoyasoma ukiwa mtoto mdogo wajua, "’Ben na Barbie,’ ah, ‘Ken na Barbie,’ sahani." "hapana, ni ‘Bertha na Barbie,’ huwezi kujua." sawa, “Bertha na Barbie wanachezea nyumba.”

Lakini, kitu ninachotaka kusema ni, Wakristo Marekani hawana msimamo wa kina kwavile kila kitu ni hufanyika kijuu juu tu …KILA KITU KINAFANYIKA KIJUU JUU. Na unasikia nabii zinazosema, “eh, eh, eh…nataka nyie mbarikiwe …na mbarikiwe ….na mbarikiwe …na vile vile mnibariki mimi .. kwakuwa mimi ni mungu wenu”

Hiyo ni nini? Huyo ni NABII WA UONGO, huo ni unabii wa uongo na huyo ni pepo anayesema “Nataka nyie mbarikiwe – ili uweze kutundikwa kwenye mtego wa mafanikio, ili uweze kumwabudu mungu wa vitu na vikorokoro, ili uweze kujilundikia, na kumkandamiza utu wako wa kiroho kwa takataka zote hizi, na unaweza kuwa Martha Stewart wa 2 kwa nyumba nzuri” na hakuna mwanaume ndani ya nyumba kwa kuwa mume ulishamfukuzilia mbali – kwavile alilitemea kapeti kahawa aliyokuwa akinywa.

Mlimbwende wa zamani unamtumia mtumba baada ya kukulipa kila kitu ulichotaka. Sugu, mgumu asiyeingilika – kwa habari ya Injili, na huku ukijidai wewe ni Mkristo … yaani kama mpumbavu, mnafiki, feki, kama vile watu wa Mungu walivyokuwa wakati Yesu alipokuja kattika mwili.

Sasa, Yeye alisema nini, au Yohana Mbatizaji aliwaambia nini? “Nyie ni kizazi cha nyoka; tubuni!” ujumbe wa Mungu sasa hivi kwa siku hii ninini? Tubu, TUBUNI, Wamarekani, kwa kiburi chenu cha MFUMO WA MAISHA. Kwanini msishushe viwango vyenu badala ya kuvipandisha? Bila shaka mna viwango vya maisha. Wala hamja…..

"Oh hapana, hapana, hapana General Deborah; umekosea. Mimi sina kipimo, siendi karibu na vipimo” Usinifanye nianze kuwa na mambo hayo. Lakini, pointi ninayotaka kuielezea ni kwamba, kitu halisi ambacho Yesu alisema ni kwamba yanakwenda kushushwa chini, nina ujumbe wenu wajenzi wakubwa, wachungaji wajenzi, batili na wachovu, na wenye magamba, na starehe na mikia ya mbwa popi, mnaojifanya: Mungu anakwenda kuwashusha chini. Ndivyo wakati wenu ujao utakavyokuwa. NDIVYO WAKATI WENU UJAO UTAKAVYOKUWA MUNGU ANAKWENDA KUWASAMBARATISHIA CHINI.

Angalia vimbunga hivi, tornado, tufani, angalia matokeo ya haya mawimbi ya tsunami wakati yanapokuja, yaangalie yote, na unaona nini? Rundo la maangamizo, rundo la uharibifu. Je, Mungu anaheshimu majengo yenu? Je, Mungu anakiheshimu kile mlichofanya?

Je, Mungu anaheshimu “nyumba yako iliyotimilifu”? Hapana, amekuachia mwanangu; sasa jioshe: UCHAFU. Alitupilia mbali uchafu ule, aliyateketeza; aliyaangamiza. Kwa hiyo hata ulimwengu wako mdogo wa mimi mimi mimi sio kitu kwake. Uthibitisho wa Mungu umetolewa … na sio kuzunguka dunia yote, umefanyika hapahapa. Mungu ameichapa nchi muipendayo sana. Mungu aiichapa arhi ya pwani, Mungu ameipiga “nchi inayotamkwa sana” Mungu ameonyesha kutokuridhishwa kwake kabisa; Mungu anaonyesha jinsi vile anavyoiheshimu sanamu za Marekani. Wacha wewe.

Na watu wako mbumbumbu na goigoi kuweza kuyaelewa haya. “Ah wakati ujao kuna nini?” naweza kukuambia: maangamizo, kuteketea, rundo la kifusi – hadi galagala kwenye kifusi kwa kunyenyekea. Nk, nk, nk. Kwanini? Kwasababu watu hawachukui hatua ya mapinduzi katika toba, kutubia kiburi chao – kiburi cha vile walivyonavyo.

Kwa hiyo Mungu anasema, "Sawa huwezi kutubu, huwezi kusogea karibu nami, vyote nitaviondolea mbali nawe, na utakaa pale na rundo lako la matakataka, na utaomboleza, na kunilaani na kufia-katika uasi wako, katika uchungu wako, na kukataa kwako wito wangu – wa kuja karibu na mimi – kwasababu hukutaka kuwa hekalu langu, kwamba ulitaka kujenga la namna uliyotaka wewe, ulitaka kufanya kama ulivyotaka, ulitaka uwe nalo ili watu wakupongeze.”

Unajua nini? Mungu hajali kama unaishi kwenye kibanda; anachojali ni kama unamtumikia kwa moyo wako wote. Na WAZO hizi tumelianzia wapi kwamba VITU vyote hivi vinatuwakilisha sisi kwamba tuko sawa na Mungu. Kama Wakristo wa Marekani wangekuwa sawa na Mungu, kusingekuwepo na harakati za mashoga.

Kama Wakristo wa Marekani wangekuwa sawa na Mungu, kusingekuwepo na vita vya magenge ya wahuni mashuleni na katika mashule ya umma zilizogeuka kuwa kambi za wafungwa – kwasababu KAMA WAKRISTO WA MAREKANI WANGEKUWA SAWA NA MUNGU, WANGETAKA SHULE ZA UMMA ZIFUNGWE. Na ningeweza kuendelea na kuendelea, na kuendelea, na kuendelea kutaja kila tatizo linaloikumba nchi hii katika saa hii; na ni kwa sababu watu wamejenga kulingana na kiburi.

Kama nilivyosema ujumbe au mbili zilizipita, “Hapa Wakristo hawa wanataka kujisifu, ‘Ndiyo, tuna vijana kanisani sasa kutoka mitaani;’ lakini umeleta umtaa kanisani” Hata mpaka wanatembea kwa majigambo sasa katika baadhi ya makanisa haya makubwa.

“Unafahamu, maeneo madogo ambapo wanawake wanaweza kuonyesha nguo zao za ndani, na viatu vyao vya umalaya, na wavulana wanaweza kuwaita, na kulegeza chupi zao nyuma, na kufanya mambo haya yote makubwa, kwa sababu vijana wako kanisani!” Hapana mpenzi, wameleta umtaa kanisani. Wala hawana thamani zaidi ya waliobakia wacheza kamari, waasherati, na makahaba, na saluni za kihuni, baa za urembo, “na labda baa mpya za vileo vikali zilizofunguliwa, namaanisha …” na kuendelea na kuendelea.

Kwanini? Kwa sababu ya kujenga juu ya uwongo, udanganyifu, kiburi, tamaa ya mwili, kiburi cha uzima----kuliko kumruhusu Mungu kujenga kwa njia yake. Hivyo Yesu akasema “Oh, makubwa, mnalo hekalu lenu; tabirini ni nini kitakachokwenda kutokea? Huo ndio uzima wako!” Je, ninyi vijana mnao msisimkokuhusu maisha yenu ya baadaye?

“Oh! ni lini tutakwenda kuanza mpango mpya wa ujenzi? Siwezi nikasubiri. Ulijua tunakwenda kuwa na kanisa la kwanza kwenye sayari ya Marsi? Litakwenda kuitwa “ Kanisa la nyota’; ungelilipenda hilo?

"Bomolewa” Alisema. “Hakuna jiwe litakalosalia juu ya jiwe jingine”. Hivyo, ni nini ufumbuzi? Tubu; TUBU njia zako, kazi zako, kiburi chako, na ukae sawa na Mungu; na MRUHUSU YEYE AJENGE. Amen.

 

 JE, UMEKWISHA OKOKA? YESU NI HALISI!! OMBA KAMA HIVI.

Mpendwa Yesu, ninakuja kwako na dhambi zote nilizozitenda na ninakuonba wewe unisamehe. Niokoe mimi kutoka kwenye maangamizo ya milele katika moto wa Kuzimu. Ninakiri kwamba mimi ni mwenye dhambi ambaye siwezi kujiokoa mwenyewe.Usiniruhusu mimi nife katika dhambi zangu. Tafadhali takasa mwili wangu, nafsi na roho kwa damu yako ya thamani.Ninahitaji msaada wako na ninakuomba wewe uje na kuishi moyoni mwangu. Nataka nikutumikie, kutii amri zako na kufanya yale ambayo ni sawa. Nataka niishi kwa ajili yako kila siku na kuupokea uzima wa milele.Tafadhali niongoze na nielekeze kwa Roho wako katika haki. Nisaidie mimi kuishi maisha safi na matakatifu yampendezayo Mungu. Asante Yesu kwa kunisikia na kunijibu maombi yangu. Amina! Soma BIBLIA!

Tuandikie kwa ajili ya kupata bure machapisho yetu mengine yanayohusu HUKUMU YA MUNGU.

Tungependa kusikia kutoka kwako!
Kuomba maandiko au taarifa zaidi kuhusu sisi au jamii yetu tafadhali tutumie E-mail:

livingword@aggressivechristianity.net

 au tuandikie:

AGGRESSIVE CHRISTIANITY
HR 60, Box 11,
Fence Lake, NM 87315


Kwa maelezo zaidi kuhusu ACMTC TANZANIA, au jinsi utakavyoweza kujihusisha, wasiliana na Meja Frank & Elina Materu: S.L.P. 7579 Dar es Salaam, Tanzania. Barua pepe: materufrank@yahoo.com